@msumbanews: Mkuu wa Mkoa wa Geita, Alexander Mnyeti, amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato kutoa gari lake aina ya Land Cruiser V8 na kulitumia kwa kubebea wagonjwa wanaohitaji rufaa katika Kituo cha Afya Muganza, baada ya gari la wagonjwa (ambulance) kuharibika matairi. Mnyeti ametoa agizo hilo wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi katika Soko la Kimataifa la Dagaa Kasenda, lililopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Chato, mkoani Geita, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kujitambulisha kwa wananchi.\ Akizungumza katika mkutano huo, Mbunge wa Jimbo la Chato Kaskazini, Cornel Magembe, amemuomba Mkuu wa Mkoa kuhakikisha ambulance ya Kituo cha Afya Muganza inapatiwa matairi mapya ili kurejesha huduma ya usafirishaji wa wagonjwa, hususan wanaohitaji kupewa rufaa kwenda hospitali. Kabla ya kuanza ziara yake ya kujitambulisha kwa wananchi wa Mkoa wa Geita, Mnyeti alianza kwa kutembelea kaburi la aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, lililopo Chato. Baada ya hapo, Mkuu huyo wa Mkoa alikutana na baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato na kuwataka kutekeleza majukumu yao kwa bidii, huku wakizingatia kusikiliza na kutatua kero za wananchi kwa wakati. Mnyeti amesema viongozi na watumishi wa Serikali wanapaswa kuelekeza nguvu zao katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na changamoto zao zinatatuliwa kwa ufanisi.
Msumba News Blog
Region: TZ
Thursday 17 September 2026 09:16:30 GMT
Music
Download
Comments
_zede1 :
This country is full of drama NGL🙌
2026-09-17 10:16:41
0
Saba :
Maigizo, ambulance ni gari maalum kwa ajili ya kubebea wagonjwa. Hilo v8 halina vifaa maalum kwa kuweza kubeba wagonjwa. Na tunashangilia.
2026-09-17 10:33:13
10
Easther Christopher🥰❤️ :
kunawatu humu wanabisha ni kwa sababu shida ni ambulance na wanaotumia ni wagonjwa ndio maana wanaona kama DED kaonewa ila mkae mkijua hata kama sio ambulance ni V8 lakin itafikisha mgonjwa kwa wakati sehemu husika ya matibabu.... KWAHIYO WAGONJWA WAFE KISA V8 SIO GARI YA WAGONJWA?
2026-09-17 11:22:52
4
Alen :
ambulance ni gari na vifaa tiba vilivyo ndani ya gari hilo
2026-09-17 11:03:43
9
TANZANITE :
lengo ni kwamba matairi ya ambulance yanapatikane haraka
2026-09-17 12:23:51
7
Medy Classic745 :
sasa iyo gari ina quality ya kuwa Ambulance? au siasa tu
2026-09-17 10:25:55
6
Larry 🎧💰 :
Et matairi hayapo tusubili ilaaaaa TZ yangu 😂😂😂
2026-09-17 10:24:53
1
Gerald Jabu1 :
Kwanini asinge agiza matairi ya humo yafunguliwe yafungwe kwenye ambulance 🚑 hiyo v8 haijatengenezwa kukidhi haja ya kubeba wagonjwa
2026-09-17 10:40:48
0
Sayuki Sheshushi :
huyu anataka sifa kwani akitoa matairi ya hiyo gari yake akaweka kwenye Ambulance shida ipo wapi mpaka atumie gari lisilo na huduma
2026-09-17 11:14:12
0
Carrasco Nation :
Mi nshukur siku hiz watanzania tunajua kuchambua uhalisia wa vitu 😂😂
2026-09-17 10:26:50
3
Addy01 :
ambulance ni zaidi ya gari. c kila gari inatosha kua ambulance. hapa issue ya ambulance ikifatiliwa vzr inaweza kuibua mengi katika mnyororo wa huduma. lkn tukiamua tu kuzima mambo kirahic hivo, tutarajie lawama kila cku
2026-09-17 10:42:41
1
Sossy :
mkuu wa mkoa kakulupuka
2026-09-17 10:45:32
0
Nick Moshi :
safi kabisa
2026-09-17 13:52:50
1
Drleon008 :
😂😂😂 jamani
2026-09-17 11:22:37
2
🆔risor2️⃣5️⃣5️⃣ :
Siasa t hizo Hilo gar kesho t lipo mtaan na mkurugenz kama kawaida dah Asa v8 inakuaje ambulance hata sifa na kitanda cha mgonjwa kitakaaje
2026-09-17 11:11:41
0
coràzone :
nilosema mkuu wa mkoa mpya n baraaa any way mbunge wetu mbona unatuzalilisha huku kwetu hii kesi hata dowan angejitolea kununia kwa pesa yake
2026-09-17 11:27:18
1
oliversteven376 :
Dramaaaa
2026-09-17 13:13:25
0
One🏹 :
apo jion ana rudishiwa v8 yake ana peleka matairi
2026-09-17 12:54:12
0
BATA POINT PUB :
ila mnyeti bwana dah
2026-09-17 12:12:47
0
Balaka Zacharia :
tungepata viongoz kama hawa 100 tu nchi ingeelewa. maana kunamkuu mja alishawahi kutamuka choo cha soko kitumike choo chakiongozi wakati anafanya mchakato
2026-09-17 11:38:49
0
MGUUWAKUTOKA :
mnashangilia kwa sababu hamjui kuwa selikali ina mifumo ya decentralization, kila kituo cha cha kutolea huduma kinajitegemea kwa kujiendesha, ni pesa chache ambazo hupangwa ndio hutumika.
mkurugenzi anahusika tu kwasababu halmashauri nzima ni yake ...
ila trust me hicho kituo watanunua mataili kwa pesa zao wenyewe, iwe kwa mkopo ama ama kwa cash
2026-09-17 17:27:37
0
CALL ME HONEYBADGE! :
kuna jambo lifuatiliwe nani ni shida hapo
2026-09-17 12:37:47
0
yanafungwa siku hyo hyo mkurugenzi ma v8
2026-09-17 15:19:02
0
senya :
@senya:pia hapo ambulance yenyewe kumbuka kibongo bongo ni landcruiser 1Hz, haina umaalumu mkubwa ambao hiyo V8 itashindwa kwa kitambo kidogo
2026-09-17 13:15:31
0
inkwale :
hapo safi sana
2026-09-17 10:17:32
0
To see more videos from user @msumbanews, please go to the Tikwm
homepage.