@kambi_health: 🚨 MAKOSA 7 AMBAYO WENGI WANAFANYA USIKU NA KUCHOCHEA ACID REFLUX Kama mara nyingi unapata kiungulia, moto kifuani, gesi, au chakula/uchachu kupanda kooni usiku, angalia haya makosa 👇 1️⃣ Kula muda mfupi kabla ya kulala Tumbo linakuwa bado linafanya kazi wakati umelala, jambo linaloweza kuongeza uwezekano wa reflux. 2️⃣ Kula chakula kingi sana usiku Mlo mkubwa huongeza msukumo tumboni na unaweza kufanya asidi ipande kuelekea kooni. 3️⃣ Kulala mara tu baada ya kula Kujilaza baada ya chakula kunaweza kurahisisha yaliyomo tumboni kurudi kwenye umio. 4️⃣ Kula vyakula vya mafuta mengi au vya kukaanga 🍗 Vyakula hivi vinaweza kuchochea dalili kwa baadhi ya watu na kuchelewesha mmeng’enyo. 5️⃣ Kunywa soda au vinywaji vyenye caffeine usiku 🥤☕ Kwa baadhi ya watu, soda na caffeine vinaweza kuongeza dalili za reflux. 6️⃣ Kula vyakula vinavyokuchochea wewe binafsi Mfano pilipili, chocolate, vyakula vyenye tindikali au vingine unavyogundua vinaongeza kiungulia. 7️⃣ Kulala bila kuzingatia mkao Kwa baadhi ya watu wenye reflux ya usiku, kuinua sehemu ya juu ya mwili wakati wa kulala kunaweza kusaidia kupunguza dalili. 👉 Usipuuze reflux inayojirudia mara kwa mara. Tambua kinachochochea dalili zako na chukua hatua mapema. 📲 Unahitaji elimu na mwongozo kuhusu acid reflux? Wasiliana nami kupitia +255 795 051 414 #AcidReflux #Kiungulia #AfyaYaTumbo #Gastritis #Heartburn

KAMBI  HEALTH ||
KAMBI HEALTH ||
Open In TikTok:
Region: TZ
Thursday 17 September 2026 10:05:53 GMT
27041
272
2
11

Music

Download

Comments

afya.yako.ni.faha
AFYA YAKO NI FAHARI YETU :
🥰🥰🥰
2026-09-18 07:25:10
1
To see more videos from user @kambi_health, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About