@dr_daniel_md: 👀 Mwili wako unaweza kukuonyesha ishara za upungufu wa damu bila wewe kujua! Kuna baadhi ya dalili tunazoweza kuziona kwenye mwili ambazo zinaweza kutufanya tushuku upungufu wa damu au upungufu wa madini ya chuma. Katika video hii nimekuonyesha ishara muhimu unazoweza kuziangalia kwenye mwili na kwa nini hupaswi kuzipuuza. 🩸 Lakini kumbuka: kuona dalili hizi pekee hakuthibitishi kuwa una upungufu wa damu au madini ya chuma. Vipimo vya damu vinahitajika kuthibitisha tatizo na kutafuta chanzo chake. Usianze kutumia dawa za kuongeza madini ya chuma bila kujua kama kweli una upungufu na sababu yake. #UpungufuWaDamu #MadiniYaChuma #Afya #DrDaniel #ElimuYaAfya