@matukioonline_tv: Wakili Mwandamizi Alute Mughwai Lissu, ambaye ni kaka wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, amekana vikali madai ya kumtumia Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Godbless Lema, kama mtu wa kati wa kumshawishi Rais Samia Suluhu Hassan ili amwachie ndugu yake. ​Ufafanuzi huo umetolewa , Septemba 17, 2026, kufuatia taarifa zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na mwanaharakati Mange Kimambi, aliyedai kuwa Alute alilipiwa gharama za malazi katika hoteli ya kifahari jijini Dar es Salaam ili kukutana na Lema kwa ajili ya mpango huo. ​Akijibu tuhuma hizo, Alute amebainisha kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote na kusisitiza kuwa endapo familia ingekuwa na haja ya kuonana na Mkuu wa Nchi, ina uwezo wa kufanya hivyo moja kwa moja bila kuhitaji mpatanishi au mpatanishi wa kisiasa. ​Aidha, Wakili huyo Mwandamizi ameweka wazi kuwa familia haijachukua hatua hiyo kwa sababu inaamini shauri linalomkabili Tundu Lissu halina msingi wa kisheria, hivyo wanasisitiza vyombo vya dola na mahakama kuacha sheria ichukue mkondo wake bila kuingiliwa na masuala ya kisiasa. "Kama sisi familia tutahitaji tumuombe Mama Samia ili amwachie, kwa nini tusiende sisi wenyewe? Mimi nina uwezo wa kwenda kwa Rais Samia, na mimi sijaenda kwa sababu kesi ni ya uongo. Nataka sheria ifuate mkondo wake. Kwa hiyo siwezi kumtumia Lema ili awe mtu wa kati kufanikisha hilo," amesema Alute Lissu. #SasaLive #AluteLissu #TunduLissu #GodblessLema #CHADEMA Arusha Tanzania

Matukionline Tv
Matukionline Tv
Open In TikTok:
Region: TZ
Friday 18 September 2026 08:56:01 GMT
390138
9406
176
156

Music

Download

Comments

abdulkaderaljabry
AOA :
Kesi ni ya Uongo. Nini maana ya TUTAKINUKISHA. ni uchochozi mkubwa sana kwa Taifa. Haina haja ya kupiga Magoti, yeye yuko Magerezani, Sheria ni msumeno, haubagui mtu. Bora ufuatilie kesi yake na Majaji. Wao ndio watoa hukumu. Kesi iko chini ya Muhimili Wao.
2026-09-18 10:27:31
35
broken.02685
WATARA ESD 419 :
wakati wa mungu ,utafika tu
2026-09-18 09:23:39
49
faizally761
faizally761 :
ikiwa kesi ni ya uongo tusubiri mahakama itoe hukumu
2026-09-18 13:33:58
8
user283844804321
simba :
kwanj mama samia ndio mahakama acheni mahakama ifanye kazi yake
2026-09-18 11:37:39
23
kingtwally
user59280824572693 :
Kwanza tukubaliane nani kamsingizia na kamsingizia nini, tusijifanye sisi ninwatoto wadogo kujifyatua kwamba lisu hajafanya kosa, lisu kafanya kosa kisheria na anajua kakosea wapi, ukweli usemwe
2026-09-18 14:08:44
10
ayoub.yusuf2
Ayoub Yusuf :
samia hana uwezo hadi mahakama itoe hukumu ama dpp afute
2026-09-18 11:29:19
13
ismailomar6105
🔵 Ismail Care TZ ✔️ :
ningekuwa ni Mimi Lisu ningeachana na mambo ya siasa nikae Nile zangu bata na familia yangu kiroho safi🥺
2026-09-18 15:08:24
17
masimbotz3
Masimbo :
mama samia anahusika vip kwenye muhimili wa kimahakama?
2026-09-18 12:16:12
5
hajimohamedy185
haji :
lisu hajashtakiwa na mama Samia hapo mama Samia anahusikaje hapo?? acheni kumchafua rais Samia acheni mahakama ifanye KAZI yake
2026-09-19 06:06:41
8
fredymafie
rapili :
𝑤𝑎𝑡𝑢 𝑤𝑎𝑛𝑎𝑜𝑛𝑔𝑒𝑎 𝑡𝑢 𝑘𝑤𝑎𝑠𝑎𝑏𝑎𝑏𝑢 𝑠𝑖𝑜 𝑛𝑑𝑢𝑔𝑢 𝑦𝑎𝑜 🤔
2026-09-18 16:31:01
4
user8722512466383
user8722512466383 :
amesema tutakinukisha jee hii hakusema? kaombeni msamaa
2026-09-19 13:01:53
4
hassanaliamur
amur :
kwahivyo tundu hakusema tutakinukisha
2026-09-19 12:13:41
4
chistowelunalaila
chistowelunalaila :
libarikiwe tumbo lililowazaa nyinyi
2026-09-18 09:22:21
17
lindah.haonga
Lindah Haonga :
mungu ampiganie lissu kama alivowapiganie paulo na sila walipokuwa gerezani
2026-09-20 04:20:37
5
christinambwambo3
Christina Mbwambo :
mbna mzee anafanana na lisu mwenyewe
2026-09-19 11:31:34
5
newisawavisa
Newisa waVisa :
Msamaha wa mwanadamu unamasharti,omba msamaha Kwa Mungu.
2026-09-19 04:24:34
6
fransisconkuyumba
fransisconkuyumba :
KING🤴 TUNDU ANTPASS LISSU atatoka tu
2026-09-19 08:30:06
2
prisca.gadiel
Prisca Gadiel :
anafanana Hadi sauti
2026-09-19 18:04:29
3
am_clipalopar
providence❣️ :
Mungu mwenye haki atampigania vita vyake.. Amina..haina hajanya kuomba kweli..mwombeni Mungu pekee...
2026-11-02 16:29:52
4
raphaelkivuyo6
raphaelkivuyo6 :
Mahakama ya tanzania haitendi haki
2026-09-19 17:20:15
1
user1923978000965
HAMIDU MPATE :
eti uwongo!!! inamaana anasingiziwa!!!
2026-09-20 06:17:23
1
user88593559995413
B.St@n :
Hii ni AI,mbona Lisu alisema atakaandani mpaka haki ipatikane.
2026-09-19 13:31:39
1
kawafrkawafr
rumaysa🧕 :
walikua wana fanana had saut jmn
2026-11-02 19:51:08
2
snipejfq2rq
Emmanuel :
sheria zipo unaenda kuomba kwani anamahakama yakee
2026-10-14 15:29:37
1
b.sultan03
b.sultan03 :
achaa serekali ifanye kazi yake haswaa mahakamaa
2026-09-21 17:40:22
1
To see more videos from user @matukioonline_tv, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About