@millardayo_: Waziri Mkuu wa Jamhuri ya MuunganowaTanzania, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, ameitaka Wizara ya Mambo ya Ndani kuhakikisha taasisi zinazojihusisha na ajira, utoaji wa huduma za kijamii na shughuli za kiuchumi zinaunganishwa na Mfumo wa Taarifa wa NIDA ili kuimarisha uhakiki wa utambulisho na kudhibiti udanganyifu na vitendo vya kihalifu. Ameyasema hayo katika hafla ya kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Utambulisho, iliyofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam ambapo ameitaka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kufikiria utaratibu wa kuwawajibisha wananchi wanaochelewa kuchukua Vitambulisho vyao vya Taifa baada ya kuzalishwa akisema Serikali hutumia fedha kuvizalisha ambazo zingeweza kuelekezwa katika shughuli nyingine za maendeleo. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, James Kaji, amesema utambulisho ni msingi wa kumwezesha mwananchi kupata haki na fursa mbalimbali za kijamii na kiuchumi. #MillardAyoUPDATES
millardayo
Region: TZ
Friday 18 September 2026 12:03:03 GMT
Music
Download
Comments
fonce kasharazi :
na sisi tunaofata na havionekani wilayani tunavifata wapi?
2026-09-18 12:49:15
218
Tashamigosi :
Nilisajili 2021 mpaka sasa ntapata kweli😅
2026-09-18 14:04:38
19
Jesca :
Mimi nilijisajili mwaka Jana mpaka leo sijatumiwa meseji
2026-09-18 13:20:02
48
Sandals chap :
Sasa mlituambia tuandike namba za simu zanini😂
2026-09-18 12:50:49
109
Ester Charles :
Waniletee si wanajua ninapoishi
2026-09-18 13:27:06
6
KIM ~LYON🥷👿 :
Mbona tukienda Wanasema hamna ? Havijatoka ?
2026-09-18 13:01:04
48
neymat💃👄 :
hebu msituchanganye ungejua wanavyoringa watu wa nida
2026-09-18 13:49:49
0
Miss lonely🫧 :
Kuna uyo mm ambaye sina hata hzo namba zenyw za nida
2026-09-18 13:56:55
12
🖤G MONEY🤍 :
vitambulisho vyenyew vinacheleeweshwa mpk leo tangu 2024 mpak leo bado
2026-09-18 13:08:01
20
JJ MULT BUSINESS :
mbona mapema sana millard
2026-09-18 12:14:28
17
Z3GG3 BOE :
Msituchanganyeee😂😂😂😏
2026-09-18 14:49:28
6
feda_official :
kwan trump amesema ananunua shngap Africa cc tutamfanyia discount TZ
2026-09-18 14:37:45
0
💦Msomali🧕💫 :
niwajibishen tu,mtu kila siku naenda et bado havijatoka,hizo naul za kupotez kila siku zinatoka wap
2026-09-18 13:17:39
9
shaaban :
Fanyeni delivery
2026-09-18 14:10:20
0
Niho17⚽️🌸 :
Nipo nje kimetoka toka 2022😂 nimeishaaa me nina namba tu
2026-09-18 12:55:19
12
Latrix_19⛎ :
Millard ayo wewe unacho 😂😂
2026-09-18 14:06:09
0
thee_drey :
Mpe bolt anileteee😂😂😂
2026-09-18 15:33:35
0
Angelina🦋 :
Mama weeeee
2026-09-18 13:04:28
0
🤍BREY🎀🫧🧸 :
mbn tunaenda kuchukua wanatuambia kila siku avijatoka jmn khaa
2026-09-18 12:57:54
7
rajose29 :
wachague kutuwajibisha au tuwaachie kabixa tusiende hata kujiandikisha
2026-09-18 12:18:18
8
eddy_tx :
Watumishi wenu wazembe hawatupatii
2026-09-18 13:07:09
4
Ms_Eve🎀 :
Uwiii
2026-09-18 13:02:19
1
Sarah 🦚 :
jamani mi nida yangu imefutika naweza kuri new au tunafanyaje maana maandishi yamefutika kabisaa
2026-09-18 13:28:30
0
Rosemary :
jamani mimi nina namba tu 😭
2026-09-18 13:03:50
0
IT’S PRECIOUS 🔐🎀🌹❣️ :
Aya njooo mnie bc ili muuue na mama angu kwa pressure pia 🥺🥺🥺🥺 sasa me nipo mbali nakipatajr na wakati siwezi kwenda uko
2026-09-18 12:52:12
5
To see more videos from user @millardayo_, please go to the Tikwm
homepage.