@innocent_raphael: Unaposikiliza mijadala ya kibunge inayohusu mipango ya maendeleo ya miaka mitano, suala la uwazi, utekelezaji wa sera, na uwajibikaji wa serikali huwa linachukua nafasi ya kwanza. Kwenye dondoo hili, Tundu Lissu anahoji uhalisia na uwepo wa mipango madhubuti ya kitaifa sambamba na kauli mbiu ya wakati huo ya "Hapa Kazi Tu", Hata hivyo alikua akisisitiza kuwa utendaji kazi unapaswa kuendana na mipango iliyopangwa tangu mwaka 2011/2012. Hii inatukumbusha dhana muhimu ya uwazi wa serikali na utekelezaji wa mipango ya maendeleo (Government Transparency and Development Planning). Mijadala ya aina hii inaleta changamoto chanya kwa viongozi kutoa hesabu za utekelezaji wa miradi na mikakati ya kiuchumi inayowagusa wananchi moja kwa moja... ila LISU 😂 kanifanya nicheke anafikirisha sana #siasa #innocentraphael #tanzaniatiktok #breakingnews