@safina.ya.mt.rith: #*NOVENA KWA MAMA BIKIRA MARIA WA MATESO SABA* *SAA LA KWANZA (1)* Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu Amina Unabii wa Simeoni Mama mwenye Mateso zaidi, Mateso yalijaa moyoni mwako wakati wa kumtolea Mwana wako wa kimungu hekaluni, Simeon Mtakatifu alitabiri kwamba upanga utachoma Moyo wako. Hapo ndipo ulijua utateseka na Yesu. Malkia wa Mashahidi, sasa niunganishe moyo wangu kwako kwa maumivu haya, na nikuombe neema ya kuweka mawazo ya kifo changu akilini, ili niepuke dhambi kila wakati. Salamu Maria.x1 *SALA KWA MAMA WA UCHUNGU KUOMBA NEEMA YA PEKEE* Ee Mama mbarikiwa na Bikira mwenye uchungu, Malkia wa Mashahidi, uliyesimama chini ya msalaba na uliyemtazama Mwana wako akifa, unitazame kwa huruma ya kimama ninayekusikitikia. Kwa sababu ya upanga uliochoma moyo wako, kwa mateso ya maisha yako nakuomba uniangalie kwa wema ukasikilize maombi yangu. Nakuomba, ee Mama, uniombee daima kwa Mwana wako, najua hawezi kukunyima wewe kitu chochote. Basi, ufanye, Moyo wa Mwanao ukubali kunijalia ombi langu hili …………………(taja ombi lako) Maana nitamkimbilia nani katika mahitaji na misiba yangu isipokuwa kwako, ee Mama wa huruma? Wewe hasa unaweza kutusaidia sisi tulio bado katika bonde la machozi kwa sababu ulishiriki mateso ya Mwanao kutukomboa. Umtolee Yesu tone moja la Damu yake takatifu. Umkumbushe ya kuwa wewe ni matumaini, furaha na maisha yetu ukanipatie jambo ninalokuomba kwa Yesu Kristo, bwana wetu. *KUMBUKA/ MEMORARE* Kumbuka, ee Bikira Maria mpole sana, haijasikilika kamwe kwamba ulimwacha mtu aliyekimbilia ulinzi wako, aliyeomba msaada na maombezi yako.Kwa matumaini hayo, nakukimbilia wewe eh Mama Mkuu wa mabikira. Ninakuja kwako, nasimama mbele yako, nikilalamika Mimi mkosefu, Eeh Mama wa neno la Mungu, Naomba usikatae maneno yangu, bali uyasikilize.... Amina. *SALI ROSALI YA MATESO SABA YA MAMA BIKIRA MARIA* *NAMNA YA KUISALI* ✝️Anza na Ishara ya Msalaba *SALA YA UFUNGUZI:* MUNGU wangu ninakutolea rozari hii Kwa ajili ya utukufu wako, ili niweze kumheshimu mama mtakatifu Bikira Maria, ili niweze kutafakari mateso yake. Kwa upole ninakuomba wewe unipatie mimi toba ya kweli ya dhambi zangu. Ninakuomba unipe mimi busara na unyenyekevu ili niweze kupokea neema na baraka ambazo zinapatikana katika sala hii. *SALA YA KUTUBU:* MUNGU wangu ninatubu Sana dhambi zangu............. Punje Tatu za mwanzo.... *Salamu Maria x3* Kwenye medali Sali Sala hii: Mama mwenye huruma tukumbushe kila wakati Kuhusu mateso ya YESU mwanao. *TESO LA KWANZA:* Utabiri wa simioni (Luka 2:25-35) kuwa moyo wa Mama Maria utachomwa kwa upanga wa mateso *Ukimya/Tafakari* *Baba yetu x1* *Salamu Maria x7* Mama mwenye huruma tukumbushe kila wakati Kuhusu mateso ya YESU mwanao *TESO LA PILI:* Mama Bikira Maria na Mtakatifu Yosefu wanakimbilia Misri usiku ili kumficha mtoto YESU asiuawe na Herode (Mt 2:12-18) Tuombe neema ili mioyo yetu iwe kimbilio Lake YESU. Mama mwenye huruma tukumbushe kila wakati Kuhusu mateso ya YESU Mwanao *Ukimya/Tafakari* *Baba yetu x1* *Salamu Maria x7* Mama mwenye huruma tukumbushe kila wakati Kuhusu mateso ya YESU Mwanao *TESO LA TATU:* Mama Bikira Maria aliona uchungu Sana mwanae YESU alipopotelea hekaluni (Luka 2:41-51) Tuombe neema ya kudumu na YESU mioyoni mwetu. Mama mwenye huruma tukumbushe kila wakati Kuhusu mateso ya YESU Mwanao Ukimya/Tafakari *Baba yetu x1…..* *Salamu Maria x7……* Mama mwenye huruma tukumbushe kila wakati Kuhusu mateso ya YESU Mwanao *TESO LA NNE:* Mama Bikira Maria aliona uchungu Sana alipokutana na mwanae amebeba msalaba (Luka 23:26-31) Tuombe neema ya kudumu na YESU siku zote. Mama mwenye huruma tukumbushe kila wakati Kuhusu mateso ya YESU Mwanao Ukimya/Tafakari Baba yetu x1….. Salamu Maria x7…… Mama mwenye huruma tukumbushe kila wakati Kuhusu mateso ya YESU Mwanao *TESO LA TANO:* Mama Bikira Maria aliona uchungu Sana alipomwona mwanae YESU anasulibiwa na Kufa msalabani (Yohana 19:25-27)Tuombe neema ya Kufa
Safina ya Mt.Ritha Wa kashia
Region: TZ
Friday 18 September 2026 13:36:51 GMT
Music
Download
Comments
Glow❤💃 :
utuombee mama maria[Pray]
2026-09-20 05:15:27
0
maria utisaidie,utuombeee Amen 🙏
2026-09-19 06:41:57
1
Tina :
Amen utuombee
2026-09-19 18:28:02
0
jacquelinejumba :
mama utuombeeAmina
2026-09-19 07:34:44
1
mary raphael :
ee mama maria utuombee
2026-09-19 06:48:21
6
Mary Mihayo :
maria utusaidie katka safar ya maisha yetu
2026-09-19 06:00:28
3
Neema Emanwel :
mama mtakatifu wamungu utuombee sisi wakosefu
2026-09-19 07:55:12
1
bad boy :
Amen 🙏
2026-09-19 09:23:30
0
Smile girl❤️❤️ :
Najiunganisha na haya maombi kwa jina la YESU🙏❤️
2026-09-20 18:19:08
0
pat Maggie :
utuombee mama maria
2026-09-20 17:12:20
0
LILTINO FASHION BOUTIQUE :
Utuombee
2026-09-20 16:49:22
0
Eunice :
mama utuombee Kwa mwanao,🙏🙏
2026-09-20 09:41:39
0
George Wainaina :
AMEN
2026-09-20 09:17:19
0
elizabethkatani63 :
UTUHURUMIE EE MAMA YETU
2026-09-20 12:24:55
0
black rose :
utuombee mama yetu
2026-09-20 11:59:36
0
Dropper Julius :
uniombe huyu kijana aliyetutapeli naamin mtakatifu lita hujawahi kushindwa aminaaa
2026-09-20 15:46:31
0
Margeret Wamaitha :
es mama Maria utuombee 🙏🙏
2026-09-20 08:24:21
0
josephy59 :
amina
2026-09-20 16:36:16
0
Mary Mwanauta :
Maria tusaidie kutufikisha kwa mwanao YESU.
2026-09-20 03:13:43
0
$sussian06@ :
Ee Mama yangu Maria uniokoe🙏🙏
2026-09-20 15:02:41
0
Ansy Sway :
amina
2026-09-20 19:17:06
0
official vinnah ❤️ :
Amina
2026-09-20 05:32:02
0
collin💞 :
Ee mama maria uniombee🙏
2026-09-20 05:15:23
0
user7778193174529 :
Ameeen mama bikira maria unilindiee watt wangu
2026-09-20 03:23:12
0
happyaloyce93 :
Ameen Ameen Ameen Ameen
2026-09-20 07:01:39
0
To see more videos from user @safina.ya.mt.rith, please go to the Tikwm
homepage.