@creatorman.og.com: Mtoto anapozaliwa huwa mara nyingi anakutana na changamoto za hasadi, uchawi pamoja na mapepo machafu.Ndomana unakuta muda mwingine mtoto analia sana usiku na kukosa usingizi kwasababu kuna vitu vibaya huwenda anaviona usiku. Tumia njia hii kumlinda mwanao asije kupatwa na hasadi, uchawi au mapepo mabaya napia aache kulia kabisa usiku kwa kutumia beti hii ambayo ndani yake kuna majina matukufu ya mwenyezimungu,yenye uwezo wakumlinda mtoto asipatwe na jambo lolote baya. NAMNA YA KUFANYA: Chukua karatasi nyeupe andika beti hii mara moja tu kwakutumia kalamu nyekundu kisha ukishamaliza kuandika isomee karatasi hiyo surat yaasin mara moja huku ukichoma ubani dhukra. Baada ya kumaliza kuisomea utaifunga karatasi hiyo na kitambaa cheusi utashona vizuri iwe kama ilizi , kisha utamvalisha mwanao katika mkono wake wa kulia au utamfunga kiunoni. Kwa hakika ukimfunga mwanao beti hii tukufu mwenyezimungu atamkinga na mabalaa mbalimbali, na atakuwa analala usiku bila kusumbua kabisa.