@jambotv_: VIDEO: Mkaazi wa Kijiji cha Ng’hambi Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma John Thomas (28), aliyefariki dunia Septemba 11 na kuzikwa Septemba 13 mwaka huu, anadaiwa kufufuliwa kupitia maombi yaliyofanywa na Nabii Isaya, kabla ya kutoweka katika mazingira ambayo familia yake inadai kuwa bado haijayafahamu. Tukio hilo linadaiwa kutokea Septemba 17, baada ya familia kusema kuwa John alianza kuwatokea wazazi wake, hali iliyowashtua na kuwafanya kumtafuta Nabii Isaya kwa ajili ya kufanya maombi. Familia hiyo inadai kuwa wakati wa maombi hayo ilimuona John akiwa amevikwa sanda nyeupe. Baada ya tukio hilo, familia inaeleza kuwa watu walianza kufika nyumbani hapo kwa wingi, ndipo Nabii Isaya alipodaiwa kuwaagiza wamfungie John ndani hadi watu watakapopungua, akisema angerudi kukamilisha alichokuwa amekianza. Kwa mujibu wa uongozi wa Serikali ya Mtaa wa Ng’ambi, baada ya taarifa hizo kusambaa, walijaribu kumpigia simu Nabii Isaya na kumtaka arudi, lakini licha ya kusema angefika, hakutokea. Hali hiyo iliwafanya wananchi kuvunja mlango wa chumba alichodaiwa kuwekwa John ili kujiridhisha, lakini hawakumkuta mtu ndani. Mama mzazi wa John pamoja na baadhi ya wanafamilia, hata hivyo, wanaendelea kusimamia madai yao kwamba walimuona John wakati wa maombi na kwamba walimbeba na kumuingiza ndani. Familia hiyo pia inasema bado ina imani na Nabii Isaya na inaendelea kuwasiliana naye kwa matumaini kwamba atarejea kukamilisha kile wanachodai kuwa ni ufufuo. Mama huyo pia anasema anaamini kifo cha mwanawe hakikuwa cha kawaida, akieleza kuwa John alianguka kwenye maji wakati wakiwa shambani kabla ya kufariki dunia. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Ng’hambi, William Samweli, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, akisema viongozi walifika eneo hilo na baada ya mlango kuvunjwa hawakumkuta John ndani. Samweli amewataka wananchi kuwa makini katika masuala yanayohusu imani, akisisitiza kuwa viongozi hawalengi kuingilia imani za watu. Amesema tukio hilo tayari limeripotiwa kwa mamlaka za juu kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Jambo TV
Region: TZ
Friday 18 September 2026 16:01:13 GMT
Music
Download
Comments
agness_tz :
when did you come Jesus
2026-09-19 00:25:52
0
Rose 🌹Mluguru 207 :
Samahan unaweza mfufua JPM tumemmiss
2026-09-18 18:57:54
15
MODERN VIEW SUNFLOWER OIL.DOM :
hiiiiii ahaaaaaa
2026-09-18 17:10:38
0
Esmark- kasusu :
mmmmmh!
2026-09-18 18:23:22
0
Hassan Manjoti :
Mnatuonaje
2026-09-18 18:15:05
1
Hamid Bakari :
He jaman mutatuua kwa uongo he
2026-09-18 20:31:31
1
maryam chiunda :
niongee kwa kusimama au kwakukaa
2026-09-18 18:27:58
3
CUTE LASTBORN WA PRIME SE🇹🇿 :
kwan wanatuonaje
2026-09-18 18:21:36
1
love 💋💋💋❤️❤️❤️ :
pole
2026-09-18 21:51:35
0
Mama Sinde :
dunia imeingiliwa jamaniiiiiiiiiiiii tuhameni dunia imekwisha hiiiii
2026-09-18 20:29:01
0
mrs teu 🥁🥁🥁🇹🇿826 :
mmmh atar
2026-09-18 21:07:37
0
Joseph Mazengo :
mpwapwa
2026-09-18 21:50:05
0
user35780877815680 :
Kwa nin hamjamuita nabii akafungua mlango yeye
2026-09-18 21:29:21
0
Ibra Truck driver... :
mwenyekit hakuona hat huo.ni uwongo mtupu haijawah tokea na haitokuj kutokea ..
2026-09-18 20:52:22
0
bajaji_point :
John gani kwanza apo?
2026-09-18 20:33:14
0
Leah :
hii media gan?
2026-09-18 19:15:10
0
Sophia kalamba :
kwa kweli wakamkuta John akiwa hayupo ila mwandishi
2026-09-18 19:03:07
0
Mama Sinde :
wame vuta familia nzima iyooo
2026-09-18 20:27:28
0
Omugonzibwa :
dunia ina mengi
2026-09-18 17:51:20
0
eng. kyoma :
Tumepigwa app
2026-09-18 16:48:36
0
happy🥰🥰 :
jamni duh 😳😳
2026-09-18 18:37:39
0
Faridi Rashidi1234 :
sanaa hiyo
2026-09-18 18:06:52
0
Apolinary Mungai Msele :
Mwandishi= Wakamkuta John akiwa hayupo
2026-09-18 17:45:27
0
Anna kyando :
Mmmh hiii ni hatariii9
2026-09-18 17:24:08
0
HONGERA MYINGA 166 :
wamechanganyikiwa awooo
2026-09-18 20:07:34
0
To see more videos from user @jambotv_, please go to the Tikwm
homepage.