@millardayo_: Kwa mara ya kwanza, Vijana 40 kutoka Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar wamefungishwa ndoa na wenza wao katika hafla iliyofanyika Msikiti Mkuu wa Paje, huku wakisaidiwa gharama za mahari kupitia ufadhili maalum. Ndoa hizo zimesimamiwa na Masheikh kutoka Ofisi ya Mufti pamoja na Ofisi ya Wilaya ya Kusini Unguja, huku miongoni mwa vigezo vilivyotumika ni kuwa Kijana awe na shughuli ya kujipatia kipato, mahali pa kuishi na Mke pamoja na uwezo wa kumhudumia kwa mahitaji mbalimbali kwa mujibu wa mafundisho ya Dini ya Kiislamu. Baadhi ya waliooa wamesema wana uwezo wa kuwahudumia Wake zao kutokana na shughuli wanazofanya kujipatia kipato, huku wakisema si jambo la aibu kusaidiwa mahari na kushiriki katika harusi za aina hiyo. #MillardAyoUPDATES