@erick.mtema: tumtakie matashi mema Leo Shirika la Mitume wa Yesu (Apostles of Jesus Missionaries - AJ) wanasherehekea miaka 25 ya Upadre (Silver Jubilee) ya Padre Henry Rimisho, AJ wa shirika hilo. Padre Rimisho alizaliwa January 26, 1969 huko Jimbo Katoliki Moshi. Baada ya kuhitimu kidato cha sita alipata wito wa Upadre na kujiunga na Shirika la Mitume wa Yesu (Apostles of Jesus Missionaries - AJ). Baada ya malezi alitumwa Chuo Kikuu Urbaniana, Italy kwa Shahada ya Kwanza ya Falsafa (Bachelor Degree in Philosophy) na kuhitimu 1996. Aliendelea na masomo chuoni hapo na kuhitimu Shahada ya Theolojia (Bachelor Degree in Theology) mwaka 2000. Mwaka 2001 alipata daraja takatifu la Upadre na akahudumu katika Jimbo Katoliki Moshi na Jimbo Kuu DSM kabla ya kutumwa Darfur, Sudan kutoa huduma za kiroho katikati ya vita. Kutokana na unyeti wa huduma hiyo alilazimika kupata mafunzo ya kijeshi ili kujilinda akiwa vitani. Katika mahojiano na gazeti la Mwananchi la Desemba 07, 2021 alisema alipata mafunzo kupitia Jeshi la Sudan. Baadaye aliendelea na mafunzo zaidi ya kijeshi nchini Kenya na Cuba hadi kufikia cheo cha Kapteni. Baada ya miaka mingi nchini Sudan, hatimaye mwaka 2007 alitumwa Chuo Kikuu Ardhi kwa Shahada ya kwanza ya Usanifu Majengo (Bachelor Degree in Architecture) na kuhitimu 2011. Kutokana na ufaulu mzuri alibakizwa chuoni hapo kama Msaidizi wa Mihadhara (Tutorial Assistant). Mwaka 2012 alitumwa tena kwa Shahada ya Umahiri ya Usanifu Majengo (Master’s Degree in Architecture) na kuhitimu mwaka 2014. Aliajiriwa chuoni hapo kama Mhadhiri Msaidizi (Assistant Lecturer) katika Idara ya Usanifu Majengo, Uchumi na Ujenzi. Mwaka 2016 alitumwa tena masomoni kwa Shahada ya Uzamivu ya Usanifu Majengo (PhD in Architecture) na kuhitimu mwaka 2021. Kwa sasa ni Mhadhiri Mwandamizi (Senior Lecturer) wa Chuo Kikuu Ardhi. Amesajiliwa na Bodi ya Wasanifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) na amesanifu majengo mbalimbali ndani na nje ya nchi ikiwemo majengo ya Kanisa. Pia ni mchezaji mashuhuri wa Karate na Judo anayeshikilia mkanda mweusi (Black Belt) katika mchezo huo. Tumtakie heri ya miaka 25 ya Upadre, Rev. Fr. Dr. Captain Henry Rimisho, AJ. Roma locuta, causa finita est 🙏🏽 #salayaleo #kwayakatoliki #catholicsongs #catholic #kanisakatoliki

Erick Mtema
Erick Mtema
Open In TikTok:
Region: TZ
Saturday 19 September 2026 04:52:51 GMT
20401
622
28
51

Music

Download

Comments

magorimyahudi4
magori :
good job padre
2026-09-19 13:42:12
0
user5207697616
user5207697616 :
ila Kanisa Katoliki
2026-09-19 12:09:52
4
limukajr2
LimukaJr :
padri anatuchanganya sasa..😂 Ni Dr, padri, mwanajeshi(komandoo), msanifu majengo....😅🫡 kwake
2026-09-19 11:20:58
3
valentinakayombo
Veronika :
Hongera sana Baba. Mu gu akutunze.
2026-09-19 16:00:20
0
nakalalo4
Nakalalo :
hongera sana padri wetu Mungu akulinde
2026-09-19 16:26:03
0
j_os_e_f
jose :
Mungu akubariki
2026-09-19 16:01:50
0
sweetmellon.08
sweetmellon.08 :
Hongera sana father,Mungu akubariki
2026-09-19 10:31:25
0
benson.sebaatian
Benson Sebaatian :
hongera sana babab
2026-09-19 16:14:50
0
joackim.vicenty
Majuto super sembe🌽🌽🌽🌽 :
hatar sn dunia inavitu vingi ambavyo hatuvijui
2026-09-19 15:38:52
0
joh32657
Joh :
Mwenye kuelewa na aelewe
2026-09-19 14:40:13
0
user9504847496517
Sam :
wale wanaosema cheo captain wamenishangaza sana
2026-09-19 11:05:27
0
pulkeriamichaeldu
pulkeriamichaeldu :
Mungu Akulinde azidi kukujalia haja ya Moyo Wako
2026-09-19 12:07:33
1
mekumeku88
meku meku :
Hongera baba
2026-09-19 11:23:09
0
mariamosha81
marina :
Hongera sana Baba Padre Rumisho kwa kutimiza miaka 25 ya ukuhani Mungu akutunze Baba uendelee kuchunga kondoo wa Mungu kwa uaminifu Amina🙏🙏🙏
2026-09-19 07:28:38
0
suraka63
suraka :
mungu azidi kumlinda
2026-09-19 10:31:25
0
green.mountain592
makundi :
sio major wa Jwtz na komandoo wa jwtz sio sahihi. Ni major na komandoo alipata huko Sudani kusini wakati akitoa huduma huko
2026-09-19 13:27:03
0
kingkatanga0
king katanga :
Ongera Sana baba mwenyez mingu akupe afya njema na utume mwema.
2026-09-19 11:01:05
0
monicasengamarwa
monicasenga marwa :
kila la kheri fr katika utumishi wako uliotukuka, Mungu mwenyezi akulinde na umutumikie kwa moyo wote kama ulivyoutoa kwake.
2026-09-19 12:38:46
0
yohanasdaughter_2
JOYLINE PETRO 🍑 :
Nchi gan hii😂
2026-09-19 16:27:02
0
maadili01
Maadili :
Mungu aendelee kusimama kwako Padre
2026-09-19 09:40:08
0
edinafefe
Edina Fefe :
mungu akulinde
2026-09-19 08:36:58
0
karengis18
Karengis1 :
Hongera nyingi sana kwake Padre Henri Rimisho, Mungu aendelee kumtunza 👏🏼👏🏼👏🏼👏🏼👏🏼
2026-09-19 08:15:25
0
user4370365328328
user4370365328328 :
Hongera sana Padre. Mungu Akujalie kuadhimisha miingine zaidi.
2026-09-19 08:04:56
0
anolddonald320
ozil :
Ambao hawajaelewa hawajasoma hadi mwisho
2026-09-19 15:07:07
0
To see more videos from user @erick.mtema, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About