@jwtz80: MAOFISA na askari wa mbwa wa vita kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliyohitimu mafunzo ya mbwa wa vita wametakiwa kuzidi kujiendeleza katika mafunzo waliyoyapata ili kuendeleza weledi walioupata katika kozi hiyo. Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Polisi wa Jeshi kwa Vikosi vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) , Brigedia Jenerali Abubakari Charo wakati ufungaji wa mafunzo ya ubobezi kwa maafisa na askari waliyohitimu mafunzo hayo katika Kikosi cha Mbwa vita 1K9 cha JWTZ. Amesema muhimu kwa maofisa na askari hao kuhakikisha wanajiendeleza katika mafunzo waliyoyapata Ili kuendeleza weledi walioupata katika kozi hiyo hasa katika masuala ya ulinzi wa amani Aidha Brigedia Jenerali Charo amempongeza Mkuu wa Kikosi cha Mbwa vita Luteni Kanali Meshark Kibubu kwa juhudi anazozionyesha katika kusimamimia mafunzo hayo kwa maafisa na askari wa mbwa vita katika jukumu lao la msingi la ulinzi wa nchi ikiwa ni pamoja na kushiriki operesheni za ndani na nje ya nchi, uokoaji na ulinzi wa amani. Naye Mkuu wa Kikosi cha Mbwa vita 1k9, Luteni Kanali Meshark Kibubu amesema kuwa anashukuru Makao makuu ya Jeshi na wahitimu wake wote kwa jinsi Jeshi linavyoweka kipaombele katika kuendeleza mafunzo ya mbwa vita ili kikosi kiweze kutekeleza dira na dhima ambayo ni kuwa kituo bora cha mafunzo kwa maafisa na askari na mbwa vita wa JWTZ wenye weledi, hodari, ujasiri na utayari wa kutekeleza majukumu ya JWTZ kitaifa na kimataifa. Aidha. Kamanda kikosi 1K9 aliongeza dhima ya kikosi ni kufundisha maafisa, askari na mbwa vita Ili walitumikie Jeshi kikamilifu wakati wa amani na wakati wa vita pamoja na Kushiriki katika Ulinzi wa Amani katika nchi zenye machafuko.

Tanzania military
Tanzania military
Open In TikTok:
Region: TZ
Saturday 19 September 2026 17:26:03 GMT
36680
1832
13
16

Music

Download

Comments

userpondelo
Pondelo :
salute soldiers
2026-09-19 19:58:18
1
user4382003842938mweke
user4382003842938 mwekezajtz :
oya wadepo Tanzania Moja mungu ibarik Tanzania
2026-09-20 08:11:07
3
ayoub.yona1
AYOUB YONA :
MUNGU ibariki Tanzanian
2026-09-20 06:43:34
1
nelly_blu7
Ancy.. :
Kazi nzuri
2026-09-20 10:22:33
0
eliapenda.mndeme
Eliapenda Mndeme :
naaipenda sana
2026-09-20 09:39:38
0
logosmollel1
Logosmollel@ :
napenda sana jeshi but nafasi hazitangazwi
2026-09-20 12:32:53
0
zumoflixtv
Bongo Ai Stories :
Bila kuchoka wanangu 🫡
2026-09-20 09:02:52
0
asasi.e.p.i
ASASI M.P :
🫡🫡🫡🫡🫡
2026-09-19 23:24:15
3
wakisu34
wakisu-34 :
💯💯💯
2026-09-19 17:32:57
1
wakisu34
wakisu-34 :
🥰🥰🥰
2026-09-19 17:32:55
1
shafiham5
shafi hamimu :
😁😁😁
2026-09-20 21:23:57
0
user033445688
fai💫✨💞 :
🥰🥰
2026-09-21 08:28:00
0
To see more videos from user @jwtz80, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About