@jamiivoice_: HABARI: Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Olivanus Thomas, ameagiza kufutwa kwa mkataba wa mkandarasi Madunda Construction na kuwataka TAKUKURU kuanza mara moja uchunguzi wa ujenzi wa barabara ya Kigasi–Milo, baada ya kubaini kasoro katika utekelezaji wa mradi huo. Olivanus ametoa maagizo hayo Septemba 18, 2026, alipofanya ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo, unaohusisha ujenzi wa barabara za zege (Concrete Strips) pamoja na makaravati. Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Mkuu huyo wa Wilaya amesema hajaridhishwa na utekelezaji wa mradi huo, akibainisha madai ya ujenzi chini ya kiwango na kushindwa kutekeleza maelekezo aliyoyatoa mwezi Machi 2026 ya kurekebisha maeneo ambayo tangu awali yalionesha kutokujengwa kwa ubora unaohitajika. Kutokana na hali hiyo, Mhe. Olivanus ameiagiza Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kuchukua hatua za kufuta mkataba wa mkandarasi Madunda Construction, huku Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ikiagizwa kuanza uchunguzi wa mradi huo mara moja. Hatua hiyo inalenga kuchunguza utekelezaji wa mradi na kushughulikia hoja zilizojitokeza katika ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya Kigasi–Milo.
Jamii Voice
Region: TZ
Sunday 20 September 2026 10:22:30 GMT
Music
Download
Comments
user4792929481773 :
mafundi mnawaacha mtaani mnachukua wamadaftari ayasasa
2026-09-20 13:42:13
0
denny22 :
jamaa sauti haitoki[Tears of joy][Tears of joy][Tears of joy]
2026-09-20 16:23:12
0
🚜 jd :
Ndio maana Watanzania hatuaminiki yani hata uzalendo zero kazi kulaumu hatupewi fursa
2026-09-20 11:24:34
45
❤️E~Money💵💫 :
Hom boy kwa heshima mkuuu💪🏾🫂🫡
2026-09-20 12:01:37
12
octavian_kangalawe :
tunakosea sana wakandarasi wa ndani
2026-09-20 14:22:09
5
Eng will🇹🇿🇹🇿🇹🇿 :
apo ukicheki GPA ipo juu, ila ukija site amna kila kitu..🤣😂
2026-09-20 14:51:51
6
Ally Naheka :
kuna mda vitu vingne vinatia hasira
2026-09-20 11:16:42
9
chk :
Shida ipo kwa viongozi aa serikali ili kuaje mpaka mtu anafika hapo mnamuangalia tu
2026-09-20 11:30:02
4
Yehosadaki Yotham :
Michezo tu mkandalasi hawez kuiba hapoviongozi balabala bilion 32 mkandalasi anapewa 20
2026-09-20 10:56:56
1
issa mjukuu :
nlipasua tair mbili hapo mahanje
2026-09-20 12:19:03
3
Abelly Mtega :
inakuaga hiv halaf baadae wanaitana ofisin wanapeana ulaji maisha yanaendelea ukitaka kuamin hilo barabara mingi zimekosewa ila hakuna iliobomolewa
2026-09-20 12:18:50
6
ronado ngoya :
eeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee.
2026-09-20 11:04:41
0
TMG TOURIST 🤏 :
niludewa yawapi hii balabla
2026-09-20 12:10:06
1
am14578 :
Tatizo kutozingatia BOQ kwa asilimia kubwa ya kuleta taharuki
BOQ inasema utaweka nondo nne kwenye beam mtu haweki hata moja anamimina tu zege kwenye box la mbao hela ya nondo imeondoka ukitwanga beam na nyundo kubwa beam lote linadondoka
watu wanaiba bila kunawa
ukiona rushwa wanataka kubwa kuliko utachofanya mradi achana na huo mradi usiwaamini wakisema sisi ndio waidhinishaji nk usiogope zigo likikudondokea huwaoni wanaingia mitini
2026-09-20 13:09:40
1
jacksonmmbando855 :
aliempa KAZI ndo shida mnacuukua MTU kisa ni chama chenu na mnafanya mambo ya aibuu mbona rzania wakandarasi wapo wengi wazuri tuuu
2026-09-20 11:45:10
0
calvin_357 :
Mkandarasi mnamuonea bure. Anzeni na procurement process mtajua hela imeenda wapi. Allegedly.
2026-09-20 16:17:16
0
B A B A W A R D A 🥲 :
hawa wakandarasi wazawa tunawatetea lkn hawajui kazi.....ni kweli wakandarasi wa nje wana piga kazi nzuri tatizo gharama kubwa
2026-09-20 13:56:31
1
Bashiru Kashumba :
Mh Dc nakupongeza kwa jitihada hizo,wakandarasi wengi wa ktanzania wanafanya kazi chini ya kiwango kama vile kazi haziwahusu wakat wanajenga miundo mbinu ya nchi yao,kisha badae haohao wanalaumu ugumu na hali mbaya ya maisha wakati wanaochangia ni watu wa aina hiyo,nikimanisha kuwa miundombinu hiyo itaharibika kwa muda mfupi na kuilazimu serikali kuleta pesa tena kufanya kazi hiyohiyo kwa muda mfupi,hao wakandarasi akifanya chini ya kiwango wafungiwe na kurudisha pesa za watu
2026-09-20 11:51:43
1
peter Machoga :
Hizo kazi unazifanya hatufuki, kunasehemu viongozi mnakosea mnakuja na camera wakati kazi zimeisha kujionesha kuwa mnatenda kazi ziro kabisa, system yako ya kazi ni ziro, hamna kitu hapo
2026-09-20 11:17:26
1
d2 :
Wamezoea kuvuruga kazi
2026-09-20 15:27:14
0
Magulu Nnyondo :
kazi za kupeana
2026-09-20 16:38:23
0
Tony genius - official :
vijana wa ssh
2026-09-20 17:16:08
0
1234567890 :
mkandalas Toka maduanda kweli
2026-09-20 16:55:13
0
Wakucheda 45 :
afungwe mhujumu uchumi huyooo[Crying]
2026-09-20 15:36:14
0
aloyceanthony467 :
10 pasenti ndo shida
2026-09-20 10:37:33
0
To see more videos from user @jamiivoice_, please go to the Tikwm
homepage.