@bongo_media: Mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, Dudu Baya, amezua gumzo kwenye tamasha la miaka 30 ya muziki wa Bongo Fleva jijini Arusha baada ya kuzimiwa maikrofoni akiwa jukwaani. Tukio hilo limetokea wakati Dudu Baya akizungumza kuhusu ushiriki wa mmoja wa wasanii kwenye jukwaa hilo, hali iliyosababisha maikrofoni yake kuzimwa. Tamasha la Bongo Fleva @30 limeendelea kuwakutanisha baadhi ya wasanii wakongwe wa muziki huo, likiwa na lengo la kusherehekea safari ya miaka 30 ya Bongo Fleva nchini Tanzania. Tamasha la Arusha limefanyika Septemba 19, 2026, baada ya awamu zilizofanyika katika miji mbalimbali ikiwemo Dar es Salaam, Mwanza na Dodoma. Dudu Baya ni miongoni mwa wasanii waliohusishwa na historia ya Bongo Fleva tangu miaka yake ya mwanzo, huku jina lake likikumbukwa pia katika matukio na mijadala mbalimbali iliyosaidia kuunda historia ya muziki huo.
BONGO MEDIA
Region: TZ
Sunday 20 September 2026 10:32:57 GMT
Music
Download
Comments
VENNA_S :
tunao mkubali dudu baya
2026-09-27 08:35:46
1
Aikatoto :
ndaro anakaz kubwa sana
2026-09-21 14:19:24
5
Ezelina :
kwani ni lazima wamuweke dudu baya? au wanajizima data..
2026-09-20 12:55:34
13
G vanny :
Dj alokuwa kwenye mtambo Anahakilia sana kitendo cha kuweka majingo na kuzima maic kabisa, maana dudu baya angeongea maneno machafu sana mpaka mkoa wa Arusha ungeathilika kutokuwepo kwa festival yoyote hapa nchini, .Dj kafanya vzr sana congraturation dj.
2026-09-21 14:27:25
3
mfezafeza :
vizuri kumzomiya maiki
2026-09-21 13:59:43
1
babuubekam :
kasusia kivipi wakat katoa show nzuri 2
2026-09-20 15:58:40
3
🌳 msuvent ⚽️ 🌳 :
surual hy dudu🔥🔥
2026-09-22 06:21:06
0
Aysher Ramadhan :
wamtoe tu
2026-09-20 16:57:55
1
Tatu Ally :
Azam huyu atakuja kuwaponza
2026-09-21 14:03:18
0
Victor :
ukweli usemwe bwana😂
2026-09-20 13:06:22
0
My Life Still My Life :
2026-09-20 20:43:57
0
Jackie😊 :
Sema nao waandaaj bhc2
2026-09-20 17:09:29
1
Mume Wangu :
sasa Kwa nn mwite
2026-09-21 07:11:53
0
MKATOLIK :
na mkubali san dudu bay yup sahii
2026-09-20 19:09:51
1
Tuty ndaga :
Wanamuitaga wa nini huyu jaman
2026-09-20 19:20:39
0
tall :
na siku mkimuacha kumuita kwenye shoo dudubaya mamba hiyo shoo mashabiki hatufiki hiyo siku
2026-09-21 21:25:47
0
aM♌️ :
Huyu wanamchukuaga wann jmn
2026-09-21 08:55:32
0
Gemini :
Leo ndo nimegundua dudubaya anatumwagwa afanye hivyo ili show itrend
2026-09-21 19:57:25
0
mamaa. Simba ubaya ubwela :
aisee uyu jamaaa😄😄
2026-09-22 12:04:27
0
Ngobei kisongoi Ngobei KiSongo :
dudu baya sizani kama anaakiri timamu
2026-09-21 12:20:47
2
Nuru Hamiss :
kwaiyo kachukia omy kukiwasha au
2026-09-21 08:58:45
0
SAM :
Kiukweli dudu baya Ukachekiwe vipimo vingine
2026-09-20 10:44:10
4
Ally mkassa :
hao wanaomuita ndo wajinga
2026-09-20 16:38:46
2
kiberengo :
mbona kavaa sare zetu
tangazo halisikia au?
2026-09-20 20:46:23
1
zabe :
🤣🤣🤣 hapo tu keshaburudisha🤣
2026-09-20 13:30:33
1
To see more videos from user @bongo_media, please go to the Tikwm
homepage.