@sauti_online: Aliyekuwa mwalimu wa Shule ya Sekondari Karansi, Wilaya ya Siha, mkoani Kilimanjaro, Omary Salum Ally, amedai kulala nje kwa siku sita yeye na familia yake, baada ya nyumba waliyokuwa wakiishi kufungwa na vitu vyao kutolewa nje kwa madai kuwa yeye si mwalimu wa shule hiyo tena. Mwalimu huyo alihamishwa kutoka shule ya Karansi kwenda Shule ya Sekondari Dahani wilayani humo, Novemba 2025, lakini aliendelea kuishi nyumba ya shule, akidai katika kituo kipya alichopangiwa ana hofu ya usalama wake. Akizungumza na waandishi wa habari, Mwalimu Omary amesema awali aliomba kuhamishiwa Jiji la Tanga, lakini ombi lake lilikataliwa na badala yake akahamishiwa Dahani, ambako anadai kituo hicho si salama kwake. "Nilihamishwa na Mkurugenzi na kukabidhiwa barua Novemba 2025,baada ya kupokea barua ile kama ilivyo ada kwa mtumishi,kuhamishwa kwanza ni jambo la kawaida kwa mtumishi,nilitii hiyo amri kwa maandishi nikaripoti katika kituo cha Dahani. Baadae tatizo lilianza katika kufuatilia haki,stahiki kwa maana ya kulipwa,hapo kukawa kuna sintofahamu nyingi. Katika ufuatiliaji huo sikuchoka baadae nikaja kulipwa Sh. 360,000 Ikatoka amri nitoke na watoto mazingira haya kama mnavyoyaona niende huko nilikopangiwa Dahani sekondari". Mimi nina hofu na hapo, nilimwambia mkurugenzi anipe kituo salama cha kazi hapo mimi ninahesabiwa ni mtoro na mpaka hapa nina mashtaka matatu,kwanza kutotii mamlaka, nikaijibu kisheria,ikaja barua nyingine maana ninaweza kuathirika daraja lakini nikasema daraja siyo kitu mbele ya uhai kama unavyoona watoto wangu mimi wadogo" Omary amesema wakati akiendelea kushughulikia malalamiko yake hayo, Septemba 12, 2026, watu waliodaiwa kutoka Utumishi. Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha, Alfred Myombo, amekiri mwalimu huyo kuondolewa katika nyumba ya Shule ya Sekondari Karansi kwa kuwa siyo tena mwalimu wa shule hiyo, hivyo nyumba hiyo ilihitajika kumpisha mwalimu mwingine aliyepangiwa kituo hicho.
Sauti Online Tv
Region: TZ
Sunday 20 September 2026 19:54:18 GMT
Music
Download
Comments
MKAMITH G :
mwl secondary
duuu we still have a long way to go.
2026-09-21 05:50:48
0
mchilo7 :
Hakuna mwalimu analilia nyumba za serikali saivi,mwl Jenga ukae kwako.
2026-09-21 02:31:03
24
Innocent Massawe :
KANUNI ZITUONGOZE TU
2026-09-21 04:56:01
0
mc_chuwa :
mwalimu mwezangu jau
2026-09-21 05:19:15
4
Dijjah🥰🥰 :
Niko nalipa 25k na umeme hapohapo ila kuajiriwa kijijini mda mwingine Raha🤣🤣
2026-09-21 05:49:05
5
Digna :
Tatizo nyumba kapange mwalimu maisha yaendelee
2026-09-21 05:44:00
4
BONGO TRANDING :
mwalimu kitonga jau
walimu wapo hawana ajira mtaani asituumize vichwa tunawaza madeni
2026-09-21 09:12:01
2
Mr. Legal 💫 :
usikute nyumba ya kupanga mikoani ni 20000 nyumba nzima
2026-09-21 04:19:58
5
venney23 :
Mtumishi wa umma anafanyiwa hivii!!!!??tena mwalimu!!!😳🙌
2026-09-21 11:00:42
2
Dabrah🦋❣️ :
mwalimu wangu wa history jamn pole😳💔
2026-09-21 08:12:16
3
Hellenlove :
huo ni uonevuu kabisaaa mwalimu ana haki zakeee kwanini mtupe vituu nje.
2026-09-21 04:23:16
4
Dr. Joshua Baraka Kungu :
huyo ni mtumishi wa umma wamemkosea sana
2026-09-21 06:43:12
0
Mazira The Great :
Hapo nahisi Mwalim Mkuu wa Shule hiyo ndo chanjo yawezekana Bifu zao binafsi au Hamtaki kwa sababu zake binafsi..... So Kuna wakati Wasimamizi wa vituo vya kazi Huwa ni wabaya sanaaa so hata hao HR walio mtolea vyombo injibya utalatibu.... Na hakuna mtumishi anae LIPWA stahiki zake kwa wakati akakataa kuhama..... Mm nacho kijua ni Halmashauri Huwa hazilizi stahiki za watumishi kwa wakati. POLE SANA
2026-09-21 05:07:40
1
linah :
kupanga nyumba nzima 30k mikoani
2026-09-21 05:16:06
0
elmandhry :
kwahiyo hapo mkweli nani
2026-09-21 05:02:22
2
H_S2026 :
watumishi wengi wanaoonewa mara nyingi ni wale wanaoonekana hohehahe. tutafute pesa wakuu
2026-09-21 01:42:48
5
ma mishe :
kujidharirisha vya bure vinamasinyango shida watumishi tunajisahau kama ipo siku tutakua so watumishi. wengine tujifunze kupitia hili tunapofanya kazi za mwajiri tukumbuke kunavikwazo vinaweza tokea so tuwekeze tunachopata.
2026-09-21 05:59:26
3
Eddo :
Basi kama kweli huyu mwalimu amelipwa stahiki zote za uhamisho hana cha kujitetea
2026-09-20 20:50:49
5
RICKY :
Huy n mtumish WA umma na nyumba NI ya umma huu sio utaratibu WA kumhamisha . akienda Ku claim alikua na pesa ndan na hazioni wahusika wanaweza kujibia?
2026-09-20 22:28:20
5
ENG Juma :
Hapo akuna haki Kwa nini watoe vitu nje wakati Sheria zipo atakama ujafika kwenye uwamisho wako wakazi Sheria zingefuata kama muajiliwa viongozi Kwa tukio kama ilo mnatufunza nini raia wenu uku nje🤔🤔🤔🤔🤔
2026-09-21 07:45:08
0
MWALIMU WA MATHE JM :
Duuh walimu wananyanyasika.
umhu anawaona. mtu mwenye uwezo wa kubadili wakinga 1000+ unamnyanyasa hvo
2026-09-21 03:17:08
1
mlinde mboje :
daaaah... utumwa wa uumma
2026-09-20 21:30:50
0
hemedilisani :
Chama cha matatizo
2026-09-21 05:01:52
1
Mwalimu ondoka kwenye nyumba ya serikali
2026-09-21 04:52:41
1
kwanini hekima hazituongozi kwenye hili
2026-09-21 04:14:31
1
To see more videos from user @sauti_online, please go to the Tikwm
homepage.