@jamiivoice_: HABARI: Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Olivanus Thomas, amemtaka mkandarasi anayejenga Daraja la Masaula, lililopo katika barabara ya Mlangali–Ligumbiro, kuhakikisha anafika eneo la mradi Jumatatu akiwa na vifaa muhimu vya ujenzi ili kuharakisha utekelezaji wa mradi huo. Agizo hilo limetolewa katika ziara ya kawaida ya mkuu wa Wilaya ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo lenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 159, ambapo alitaka mkandarasi kuzingatia ratiba ya kazi na kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya miundombinu inayokusudiwa. Akizungumza katika eneo la mradi, DC Olivanus amesisitiza umuhimu wa mkandarasi kupeleka vifaa muhimu kwa wakati, akieleza kuwa upatikanaji wa vifaa ni sehemu ya msingi ya kuhakikisha shughuli za ujenzi zinaendelea bila vikwazo visivyo vya lazima. Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa Wilaya amewataka wakandarasi wazawa wanaopata zabuni za miradi ya maendeleo kuwa wazalendo na kutekeleza majukumu yao kwa uaminifu, akisisitiza kuwa wanapopewa fursa za kazi wanapaswa kuonyesha uwezo na uwajibikaji ili kuondoa malalamiko yanayoweza kujitokeza kuhusu utoaji wa zabuni kwa wakandarasi wa ndani. Amesema utekelezaji wa miradi ya maendeleo unahitaji ushirikiano, uwajibikaji na kuhakikisha fedha zinazotengwa zinatumika kwa kazi iliyokusudiwa, huku akisisitiza kuwa ujenzi wa daraja hilo unapaswa kuzingatia viwango vinavyotakiwa. Katika ziara hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Ludewa aliambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Ludewa, kwa ajili ya kukagua maendeleo ya mradi na kujiridhisha na utekelezaji wa shughuli za ujenzi katika eneo hilo.
Jamii Voice
Region: TZ
Sunday 20 September 2026 20:34:41 GMT
Music
Download
Comments
mursally de,ayo :
kwani mtu ukishatoa contract unaruhusiwa kuuliza tena kuhusu vifaa au unatakiwa ukabidhiwe kaz
2026-09-21 07:15:58
4
Mr pikipiki :
unprofessional judgement
2026-09-21 04:22:18
5
dady :
kesi Isha kuà ngumu
2026-09-21 04:33:25
2
lido :
kiongozi safi sana tunataka namna hii kiongozi kysimammia fedha za walipa Kodi hamsha hao wafanyae kazi
2026-09-21 08:40:34
0
janaba :
Mimi siwezi kumjibu yeye sio fundi, kama muda wa site umeisha niliopewa ana haki ya kunihukumu, lakini kama muda bado ninao🙌 tunakiwasha tuu
2026-09-21 06:18:47
0
MODERN CAR INTERIOR :
sema kimeumana
2026-09-21 08:40:10
0
kemo Tz 🇹🇿 :
fundi anatoa macho tu
2026-09-21 07:28:59
0
jpm baba :
😂😂😂😂Hadi nacheka
2026-09-21 08:40:06
0
beyondphaseone :
hapo ni ludewa sehemu gani
2026-09-21 08:54:10
0
b7 :
fundi anashangaa iyo leo iyo
2026-09-21 07:50:55
0
CHARLZ :
kwan mnatumia sim gan mbona camera hivyo
2026-09-21 07:23:42
0
Boss :
ingekua pesa mnalipa kama mnavyo sumbua watu saiti ingekua lamaana sana
2026-09-21 07:05:25
0
kill boy :
mi niko bizeee
2026-09-21 00:38:44
0
SHUNNY VIFAA VYA UJENZI :
Huyu ndio mkuu wangu wa wilaya hanaga ubabaifu amenyooka hatari
2026-09-21 05:22:44
0
kemo Tz 🇹🇿 :
safi sana tunahitaji viongozi kama hawa hatutafanya vitu vya ubabaishaji
2026-09-21 07:26:09
0
Shariff Anan :
classmate kikaangoni
2026-09-20 21:32:34
4
kishavu :
hela za mama mnazichezea
2026-09-20 22:01:30
1
Theop Tkl :
kazi nzur baba
2026-09-20 20:45:16
1
user8722512466383 :
iyo ndio kazi ya usimamizi wa majukumu yako mkuu hongera
2026-09-21 08:48:53
0
David Raphael :
mikwara mingi tuuu hamna lolote ...mkali wa hizo show alikua ni JPM
2026-09-20 21:53:56
11
Bakunta :
Dogo ametia mikono mifukoni ila GenZ bana 😂😂😂
2026-09-21 03:45:15
4
PAPE BRAND FASHION 🔥✅ :
Kawasha fulu 😳
2026-09-21 04:34:18
1
Eustace :
katoa macho kinoma yani
2026-09-21 03:47:41
2
Sunday Umeme ⚡⚡ :
huyu anataka cheo tuuu hpo
2026-09-21 10:17:12
0
Startamu Senyagwa :
njooo kilosa
2026-09-21 07:44:11
0
To see more videos from user @jamiivoice_, please go to the Tikwm
homepage.