@innocent_raphael: Viongozi hutumia lugha ya picha, utani, na uhusiano wa kijamii kujenga daraja la ukaribu na wananchi wao. Video hii, tunasikia kauli yenye mchanganyiko wa utani na msisitizo kutoka kwa Hayati Rais Dkt. John Pombe Magufuli (JPM). Aliposema "Lakini hata sura yake nzuri... unajua sisi Wasukuma tunapenda weupe... Unapokuja, msaidizi wako ni mweupe hata kama ulikuwa una stresu ofisini inapotokea." Kauli hii inatukumbusha namna utani wa kitamaduni na kisiasa unavyoweza kutumika kupunguza msongo wa mawazo na kuleta mshikamano katika hadhara. Kama alivyowahi kuchambua mwanafalsafa na mtaalamu wa sosholojia Pierre Bourdieu katika nadharia yake ya mtaji wa kijamii na utamaduni, namna viongozi wanavyowasiliana na jamii kupitia lugha za asili na utani wa kijamii huchangia kwa kiasi kikubwa kuleta hisia za ukaribu na kukubalika. INAENDELEA.... USIKOSE #siasa #innocentraphael #tanzaniatiktok