@mainlandgrouptz: Mainland Group ambao ni watengenezaji wa mafuta ya kupikia ya Sunland na Merrin Farm, wameonesha nia ya kuwa Wadhamini Wakuu wa shindano la Pika Challenge (@pikachallenge). Mkurugenzi wa Mahusiano wa Mainland Group (@mainlandgrouptz), Betty Mkwassa amekutana na Mkurugenzi wa Fresh Ideas, Solomon ambao ni waratibu wa Pika Challenge na kubadilishana mawazo kuhusu namna ya kushirikiana kuhakikisha shindano hilo linafanyika kwa mafanikio makubwa. Solomon ameishukuru Mainland Group kwa kuonesha kuthamini vipaji vya Watanzania, huku akiendelea kuwakaribisha Wadau na Wadhamini wengine kuungana na Pika Challenge. Wadau wanaotaka kushiriki au kudhamini Pika Challenge wanaweza kuwasiliana na waandaaji kupitia namba 0759 433 006.#familyfood #SunflowerOil #cookingoil #pikachallege