@ntvkenya: Kenyatta Apata Uhuru Wa Siasa: Mahakama Kuu imempa rais mstaafu Uhuru Kenyatta ushindi wa kisheria. Hii ni baada ya kutangaza kuwa vifungu vinavyolenga kumnyima mkuu wa zamani wa nchi marupurupu yake ya kustaafu au kumzuia kushikilia wadhifa katika chama cha kisiasa vinakiuka katiba. #NTVJioni