@kalunde.health.so: VITU VINAVYOWEZA KUSABABISHA HEDHI KUBADILIKA-BADILIKA ๐น Mvurugiko wa homoni โ unaweza kufanya hedhi iwahi, ichelewe au ikosekane. ๐น Msongo wa mawazo (stress) โ huathiri homoni zinazohusika na mzunguko wa hedhi. ๐น Kubadilika kwa uzito โ kuongeza au kupunguza uzito kwa haraka kunaweza kuvuruga mzunguko. ๐น PCOS โ hali inayoweza kusababisha hedhi kuwa chache, nyingi au kutokea bila mpangilio. ๐น Matumizi ya baadhi ya njia za uzazi wa mpango โ kama sindano, vidonge au P2 yanaweza kubadilisha mzunguko kwa baadhi ya wanawake. ๐น Mimba โ kuchelewa au kukosa hedhi kunaweza kuwa mojawapo ya dalili za mwanzo za ujauzito. ๐น Mazoezi makali au mabadiliko makubwa ya ratiba ya maisha yanaweza pia kuathiri mzunguko. โ ๏ธ Kama hedhi yako imebadilika ghafla, inakosekana mara kwa mara, inakuwa nyingi sana au una maumivu makali, ni vizuri kupata ushauri wa mtaalamu wa afya.
kalunde health solution
Region: TZ
Monday 21 September 2026 17:05:41 GMT
Music
Download
Comments
There are no more comments for this video.
To see more videos from user @kalunde.health.so, please go to the Tikwm
homepage.