@uwaktatz: إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ INNALILLAH WAINNA ILAYHI RAJIUWN HAKIKA SISI NI WA ALLAH NA KWAKE TUTAREJEA. Kwa masikitiko makubwa, Umoja wa Wahadhiri wa Kiislamu Tanzania (UWAKTA) umepokea taarifa ya kifo cha Bi. Fatma Karume, aliyekuwa mjane wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Marehemu Mheshimiwa Abeid Amani Karume. Bi. Fatma Karume amefariki dunia usiku wa 21 Septemba 2026, Zanzibar. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, Swala ya Janaza itaswaliwa katika Msikiti wa Jamii Zenjibaar majira ya Alasiri tarehe 22 Septemba 2026, na marehemu atazikwa Mbweni katika Makaburi ya Familia. UWAKTA inatoa salamu za pole na rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa na wote walioguswa na msiba huu. Tunamuomba Allah SWT amsamehe marehemu makosa yake, amrehemu, ampanulie kaburi lake, amjaalie nuru ndani yake, na amuingize katika Jannatul Firdaus. Tunamuomba Allah awape subira, nguvu na faraja wafiwa katika kipindi hiki kigumu. اللهم اغفر لها وارحمها وعافها واعف عنها Amin Ya Rabbal-'Alamin. UMOJA WA WAHADHIRI WA KIISLAMU WA TANZANIA (UWAKTA)
UMOJA WAWAHADHIR WAKIISLAMU TZ
Region: TZ
Tuesday 22 September 2026 05:53:25 GMT
Music
Download
Comments
ROYAL PRINCE :
allahu ampe gauli thabit
2026-09-22 06:58:11
1
Suleiman Abdulrahman :
Io aya apo juu umeikosea kitaratibu za uandishi wa qur -aani
2026-09-22 07:34:19
0
UKHTY ZK :
Innalillah Wainna lillah Rajiun
2026-09-22 11:59:08
0
subira :
radhwiyallah anuh
2026-09-22 07:52:09
0
babuu :
poleni.sana.ndugu.zangu.katika.imani.kwa..kumpoteza.bibietu.allah.ampe.makazi.mema.huko.enndako..amueke.palipo.na.wanawake.wema🤲
2026-09-22 10:04:55
0
soba ussibasha :
kaluuu Innaliahiwainaillahirajiun Allah amsamehe makosa yake
2026-09-22 07:34:41
0
To see more videos from user @uwaktatz, please go to the Tikwm
homepage.