@rashidbattashy: KAULI YA RAIS MWINYI NA OMO BAADA YA UAPISHO LEO IKULU, ZANZIBAR YAFUNGUA UKURASA MPYA WA KISIASA โœ๐Ÿป @rashidbattashy Baada ya takriban miezi 11 ya kusubiri tangu kukamilika kwa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, Zanzibar leo imefungua ukurasa mpya katika mchakato wake wa kisiasa, baada ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, @dr.hmwinyi , kumwapisha @othmanmasoudothman kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar. Hafla ya Kuapishwa kwa Othman Masoud imefanyika Ikulu ya Zanzibar, ikiwa ni hatua inayokamilisha nafasi ya Makamu wa Kwanza wa Rais katika muundo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Othman Masoud, ambaye pia ni Mwenyekiti wa @actwazalendo_official , amerejea katika nafasi hiyo baada ya chama chake kukubaliana kushiriki katika mchakato wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa kufuatia mazungumzo ya kisiasa yaliyofanyika kwa kipindi cha miezi kadhaa. Mchakato huo ulifuatia hali ya kisiasa iliyojitokeza baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, ambapo ACT-Wazalendo haikuwasilisha mara moja jina la mgombea wake kwa nafasi ya Makamu wa Kwanza wa Rais. Hatua hii inatajwa kuwa sehemu ya utekelezaji wa mfumo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa na makubaliano ya kisiasa yaliyofikiwa kati ya @ccmtanzania na ACT-Wazalendo. Katika nyakati tofauti, Rais Dkt. Hussein Mwinyi pamoja na Othman Masoud wamezungumzia umuhimu wa mazungumzo, maridhiano na kuweka mbele maslahi mapana ya Zanzibar na wananchi wake katika kipindi hiki kipya cha kisiasa.

Rashid battashy
Rashid battashy
Open In TikTok:
Region: TZ
Tuesday 22 September 2026 10:25:29 GMT
15806
559
19
66

Music

Download

Comments

d.star864
#D STAR๐ŸŒŸ :
but mwiny kanuna mbn
2026-09-22 15:33:16
4
armaanalimkubwa
TONI :
njaa itatuua
2026-09-22 11:40:51
5
user4511867707963
Muufai :
Kuna kitu nimeona ila stiiii neno Allah awafanyie wepes inshallah
2026-09-22 14:43:51
7
fmingo4
SAFFRON :
Mbona Mwinyi kanuna?
2026-09-22 15:30:09
3
binyahya_34
Yahya Al Zenjibar :
hatakiwi hapo kukenua wala kucheka ndo mana mwinyi kanuna
2026-09-22 16:29:15
3
saleemhemedy
Saleem Hemedy :
amefika bei
2026-09-22 19:05:29
0
bazaar997
BAZAAR :
kbsaaa apo sitatoa siri๐Ÿ˜…๐Ÿ˜๐Ÿ˜‚tushapigwa kitu kizitoo
2026-09-22 13:28:17
3
lamu.taxidriver
LAMU TAXI DRIVER :
kuna siri uko
2026-09-22 12:55:57
1
rahmaqfbu2y
Rahma :
Allah atufanyie wepes inshaallah
2026-09-22 18:53:39
0
zaka.tours.safaris
Zaka tours & Safaris ๐Ÿฌ๐Ÿฆ’ :
Yaan anauhakik uchaguz ulikua batil leo anaapia serikali ya CCM duh!! ๐Ÿฅฒ
2026-09-22 19:00:00
0
omar.salim500
MAISHA YANA SIRI KUBWA :
Omo mshaur baba Hosseini Ali mwinyi kuwa vijana bado hawaja pewa hak saw hasa hususan upande wa kiume
2026-09-22 19:39:21
0
mam.h32
mam.h :
kumbe hii nchi ilikua hainaa makamo wa kwanza au
2026-09-22 19:40:39
0
user63800349531482
ู…ุญู…ุฏ ุณู„ูˆู… ุงู„ุบูŠุซูŠ :
safi
2026-09-22 12:33:46
0
hassanzanzibar7
HMKT ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ๐Ÿ‡ฎ๐Ÿ‡ณ :
๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘
2026-09-22 10:36:07
0
bilalmakame
Mr B :
๐Ÿ˜ณ
2026-09-22 16:30:23
0
To see more videos from user @rashidbattashy, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About