@openonlinemedia: Sakata linalohusu jezi mpya za Timu ya Taifa ya Tanzania ((Taifa Stars), limeingia katika sura mpya baada ya Kampuni ya Sandaland Fashion Wear Limited kutangaza nia ya kuchukua hatua za kisheria dhidi ya kauli iliyotolewa kuhusu jezi hizo. Kampuni hiyo, kupitia jopo lake la wanasheria linaloongozwa na Wakili Cletus Nziku, imesema kauli hiyo imeathiri jina, hadhi na taswira ya chapa yake, pamoja na uaminifu wa wateja wake. Akizungumza na waandishi wa habari, Wakili Nziku amesema Sandaland imewasilisha barua kwa muhusika ikimtaka kurekebisha kauli hiyo na kutoa radhi, akieleza kuwa kampuni imeona kuna madhara yaliyoweza kujitokeza kwa biashara na taswira yake. Kwa mujibu wa Sandaland, jezi hizo zimetengenezwa na kusambazwa kwa kuzingatia mkataba uliopo kati ya kampuni hiyo na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), huku ikisisitiza kuwa inaendelea kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa masharti ya makubaliano hayo. Wakili Nziku amesema suala hilo linapaswa kutazamwa katika muktadha wa mkataba kati ya Sandaland na mteja wake, akisisitiza kuwa kampuni haijaacha kutekeleza wajibu wake kama ilivyokubaliwa. Kwa sasa, kampuni hiyo imesisitiza msimamo wake wa kutaka kauli hiyo irekebishwe na muhusika kuomba radhi, huku ikionya kuwa kushindikana kwa hatua hiyo kunaweza kulazimisha suala hilo kupelekwa katika vyombo vya sheria. #Pakua App ya #OpenMedia playstore kusikiliza #DoubleORadio na kutazama #OpenMTV au kupitia tovuti #openmedia.co.tz, Kwa Matukio, Habari na Matangazo wasiliana nasi 0677107271 au 0677107273.

Open Online Media
Open Online Media
Open In TikTok:
Region: TZ
Tuesday 22 September 2026 16:48:25 GMT
145
13
0
0

Music

Download

Comments

There are no more comments for this video.
To see more videos from user @openonlinemedia, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About