@finishingmaster: MAFUNDI, ACHENI TABIA YA KUMWAGA RANGI CHOONI! 🚨 wengi, hasa mafundi wa rangi, wana tabia hii mbaya sana ya kumwaga rangi chooni. Wakati mwingine fundi anakosea mahesabu kabla ya kununua rangi. Kazi ni ndogo, lakini ameagiza rangi nyingi. Badala ya kusema ukweli kwamba rangi imebaki, anachukua mabaki ya rangi na kuyamwaga chooni ili kuondoa ushahidi. Baadaye anasema: "Boss, rangi imeisha. Ongeza nyingine." Wakati kumbe sehemu ya hiyo rangi aliimwaga mwenyewe chooni. Lakini kuna wengine wanafanya hivi kwa makusudi kabisa kwa ajili ya kumkomoa boss au tajiri. Mmezozana, mmegombana au kuna jambo limewakera, basi anasema moyoni: "Kama umenikosea, nitakutia hasara." Anaichukua rangi na kuimwaga chooni, halafu anadai rangi imeisha ili boss anunue nyingine. Hii ni tabia mbaya sana. Na wengine wanafanya kwa uzembe na uvivu. Muda wa kazi umefika mwisho, fundi anataka kuondoka, rangi bado ipo nyingi na hajamaliza kazi. Badala ya kuhifadhi rangi iliyobaki vizuri, anaimwaga chooni ili ionekane kama rangi imekwisha. Hii siyo professionalism. Kama una tatizo na boss, zungumza naye. Kama umefanya makosa kwenye mahesabu, sema ukweli. Kama rangi imebaki, ihifadhi. Usimdhulumu mtu kwa sababu tu wewe umefanya kosa au umeudhika. Na kumbuka, kumwaga rangi chooni kunaweza pia kuleta matatizo kwenye mfumo wa drainage na kumuongezea mteja gharama nyingine. Mafundi wengine wanapofika kwenye kipindi ambacho kazi hazipatikani, wanaanza kulalamika: "Kazi hakuna..." "Maisha magumu..." "Wateja hawapatikani..." Lakini wakati mwingine tunapaswa pia kujiangalia wenyewe na tabia tunazofanya kwenye kazi. Usimdhalimu mtu asiye na hatia halafu ukategemea kila kitu kiende vizuri kwako. Uaminifu kwenye kazi ni sehemu ya taaluma. Fundi mzuri si yule anayejua kupaka rangi vizuri tu. Fundi mzuri ni yule anayeheshimu material ya mteja, anakuwa mwaminifu na anaacha kazi ikiwa salama. Kwa hiyo mafundi wenzangu, hasa mafundi wa rangi: ACHENI TABIA YA KUMWAGA RANGI CHOONI. 🚫 Usimkomoe boss kwa kumtia hasara. Usifiche makosa yako kwa kumwaga material. Usifanye uzembe kwa sababu tu unataka kuondoka. Jenga jina lako kwa uaminifu, ubora na nidhamu ya kazi. FINISHING MASTER — Ubora wetu ni alama yetu.

Finishing master
Finishing master
Open In TikTok:
Region: TZ
Tuesday 22 September 2026 18:14:22 GMT
242192
5041
246
432

Music

Download

Comments

remishawa333gmail.com
Remi shawa :
Hayo nimaji sio rangi
2026-09-22 18:53:11
95
jah.ki10
Jah ki :
fundi professional haibi anakuibia kwenye quotation only
2026-09-23 07:48:17
0
officialezra_pro
Officialezra💎 :
mabosi Kuna muda wanazingua unakuta saiti Ina macamera afu Sasa boss nae ana mikwara mara atoke na bastora anaifuta mbele Yako af anakwambia rangi ikibaki anakukata kwenye hela Yako ya ufundi we unafanyeje na ndo rangi imebaki rangi isipotosha anakwambia utajua pa kuzipata rangi ,
2026-09-22 18:55:35
92
_makole
makole 🇹🇿 :
mi nifundi sjawahi kuwaza kuwa kuna fundi anaweza kufanya hivi du nimeshangaa
2026-09-22 18:44:48
57
gaudesia.nicholau
G. Nick :
tunao uza Hardware tunaelewa tabia zao
2026-09-23 07:58:38
26
chusse07
CHUSSE JR :
sorry bro some times inakuwa hiv boss anamwambia fundi atasimini rangi za nyumba nzima sasa fundi some times huwa anazidisha kwasababu zikipungua akimwambia boss boss ataona ameibiwa Kwaiy zinazobaki zile zile wanaamua kumwaga
2026-09-22 20:07:57
24
sherackbishaza
mr78 :
sasa Kam hautaki kumlipa afanyeje
2026-09-22 20:28:25
17
maria.mashishi42
Mis🤫SiLenCe⭐🌍 :
🤣🤣🤣🤣🤣usituthemeeeee please🤣🤣🤣
2026-09-22 21:17:07
0
idreamfoto
Chakas 🌱 :
Comment imejaa mafundi wanahalalisha hiki kitendo 😂
2026-09-23 04:42:45
11
salama.maliki
سَلَامَة عَبْدُ الْمَالِكِ :
hii ni zaidi ya roho mbaya
2026-09-22 20:04:13
40
maryneychelsea_
Maryney Chelsea :
This is wickedness!!
2026-09-22 22:16:46
1
jd_6575
🚜 jd :
Narudia yale yale Watanzania hatuaminiki ndio maana hata fursa za miradi mikubwa wanapewa wageni ila kulalamika 1000%
2026-09-23 03:38:25
21
goodluckmbungwe
goodluck mbungwe :
sasa kama bosi aondoki ameganda getini mm nifanyaje nimefanya sana tu.
2026-09-23 05:00:32
5
billionaire0724
Billionaire :
unasemea langi kunabati zimepigwa mbili mbili baada boss kuwabana wasiibe Yan mafundi
2026-09-22 21:08:01
8
ms_elizer13
Elizer🎀 :
Oooh kumbe ss sitajenga choo mpk kaz ioshe
2026-09-22 19:58:22
6
michellesaronga
michellesaronga :
kuna fundi amejenga nyumba nyingi sana kubwa na za kifahari ila yeye aliishia kupanga kijumba cha ajabu [Innocent]
2026-09-23 04:10:33
5
gide_elias
gidel tz :
sio wote tutashika pesa,wengne watashika adabu
2026-09-22 19:34:19
5
consolatanyambe
consolatanyambe :
ni kweli wanafanyaga hivi, ht me niliwahi shuhudia
2026-09-23 11:22:10
2
mkingawellidng
mkingawellidng :
Daaaaaa siopoa
2026-09-22 19:05:27
6
user38663630823273
[email protected] :
Bora aibe akatumie kuliko kufanya hivo
2026-09-22 19:05:30
5
gkconstruction53
GK construction🏗️💪 :
unamwaga hela .bora uziache hapo saiti ili ikichafuka unarudishia bos unakuona bora
2026-09-22 18:51:26
7
maria.mashishi42
Mis🤫SiLenCe⭐🌍 :
mabosi wanakeragaa sanaaa hujui tuu😂😂😂😂😂
2026-09-22 21:17:35
4
yussamsuleiman
yussamsuleiman :
iyo rangi tajir ni maji yaliotumik kuloweka lola na brash z kupakia rangi😂🤣
2026-09-22 21:05:38
2
tcnajma32
Najma :
sasa wakibakiza mnawasema wakibeba ni wezi ,wakimwaga laana
2026-09-23 05:03:16
1
rhea_itgirl
It girl(rhea)🫶 :
Mine nilikuta cement imemwaga nyuma ya nyumba imekorogwa ni Kama mifiko 5 ya cement 😂
2026-09-23 13:42:48
1
To see more videos from user @finishingmaster, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About