@jambotv_: VIDEO: Katika mwendelezo wa mawasilisho ya mwisho (final submissions) katika kesi ya uhaini namba 19605/2025 inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Antiphas Lissu, Lissu ameeleza jinsi upande wa mashtaka (Jamhuri) ulivyojichanganya na kuleta mashahidi wenye kauli zinazokinzana kuhusu nani aliyealika waandishi wa habari katika mkutano wa Aprili 3, 2025. Akiwasilisha uchambuzi wake wa kisheria mbele ya jopo la majaji watatu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, Lissu amesisitiza kuwa mgongano huo mkubwa kati ya mashahidi wa serikali unayafanya maelezo yote ya Jamhuri juu ya suala hilo kuwa "ushahidi usiokuwa na thamani yoyote". Katika taarifa ya ziada iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) wakati wa usikilizaji wa awali (preliminary hearing - ukurasa wa 131 wa rekodi za mahakama), Jamhuri ilidai kuwa Tundu Lissu ndiye aliyealika waandishi wa habari kutoka vyombo vya habari kama Jambo TV, Clouds Media, na Mwananchi katika mkutano wa watia nia Makao Makuu ya CHADEMA Mikocheni. Lissu amefafanua kuwa tuhuma hii haikuwa ya bahati mbaya, bali ilipangwa kimkakati ili kuthibitisha kile kinachoitwa "tendo la wazi" (overt act) la kisheria linalohitajika ili kuthibitisha kosa la uhaini. Amesema kisheria ikiwa mtuhumiwa ndiye aliyealika waandishi wa habari ili hotuba yake irushwe, kitendo hicho kingetumiwa kama thibitisho la nia ya kihaini. Zaidi ya hayo, kingewafanya waandishi wa habari waliohudhuria au kurusha matangazo hayo kuchukuliwa kama washirika walioingia kwenye kosa la kuchepusha, kuwezesha au kunyamazia uhaini (misprision of treason) linalobeba adhabu ya kifungo cha maisha gerezani.
Jambo TV
Region: TZ
Wednesday 23 September 2026 18:09:53 GMT
Music
Download
Comments
elim ni tam balaa mungu atujaliye maisha mema tusimeshe qatoto wetu
2026-09-24 09:32:28
0
Mboje masanja Zelemani :
jamani wtz tusomesheni watoto
2026-09-23 19:12:31
3
emanuelsarwatt :
lisu ni Simba na ni mfalme wa nyikani
2026-09-24 08:08:03
1
jovin com :
nice
2026-09-23 22:18:12
1
ambianzi shituka :
baba kwann ukunisomesha kumbe elimu ndo tamu hivi
2026-09-23 20:08:48
0
Emperor👑👑 :
hiv sihawahawa wanaotupasha ndo Jambo Tv😂😂😂
2026-09-24 05:48:33
2
mwakimtha mbilinyiamigo329@gma :
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
ila kunamtu akili yake anaitumia vizuri sana
2026-09-23 19:00:47
2
To see more videos from user @jambotv_, please go to the Tikwm
homepage.