@jaymusic255: MAKOSA KIFRIKA KATIKA WIMBO WA PROF JAY “NIKUSAIDIAJE” Nikusaidiaje ni wimbo ulioandikwa na msanii wa bongo flavor anayekwenda kwa jina la prof jay akimshirikisha ferooz ni matumaini yangu wengi humu ndani mnafahamu kibao hiki kilichovuma miaka ya 2003-4. wimbo huu unamaudhui kuhusu kijana wa mjini ambaye baada ya kwenda kijijini kusalimia anakutana na msichana mzuri kwa jina la zubeda, anatokea kumpenda anafanya mipango ya kumwoa kisha kuja naye mjini. Lakini binti baada ya kuja mjini anabadilika tabia na anaishia maisha mabaya. Baada ya kuusikiliza kwa kina mashairi ya wimbo huo naweza kubainisha mambo yafuatayo juu. Kukubali kuwajibika. Katika mashari ya wimbo huo mwanzo mwisho anasikia prof akirusha lawama zake kwa zubeda kuwa yeye ndio chanzo cha masaibu yote yaliomkuta, Lakini tukitazama kwa undani Zaidi tutagundua ya kwamba chanzo cha yote ni prof jay mwenyewe kumchukua binti wa kijijini na kumleta mjini. Inatambulika kwamba mazingira yanaathiri watu kitofauti kutokana na constitutional ya miili yao sasa kwa bahati mbaya binti zubeda hakuweza kustaimili mambo ya mjini jambo ambalo ni la kawaida. Kama prof hakutaka binti asiharibikiwe asibadilike basi yeye ndo angehamia kijijini. Na hii kutokuwajibika inahusu pia kuwaacha mashangingi yamdanganye bila kuchukua hatua yoyote. Upande wa pili. Katika wimbo huo tunasikia upande mmoja tuu wa mwandishi ukieleza kilichotokea juu ya mahusiano baina ya mwandishi wetu na zubeda upande wa zubeda hamna kabisa. Kutokana na hilo Napata wasiwasi inawezekena baada ya kumleta mjini binti wa watu yeye akawa anamwacha peke yake nyumbani ili kukwepa aibu kwa washikaji zake kwamba mke wake mshamba, na hii inatokana na kipande kimoja kudai kwamba yeye “nilipokuwa natoka naye nyuma anatoka” wanahadhira tungependa kujua alikokuwa akitoka alikuwa akielekea wapi? Mchezo wa sandakarawe. Mwandishi wetu amesahahu kabisa kwamba kwenye maswala ya ndoa ni sandakalawe kuna kupata na kukosa, sasa yanini kutupa lamama hasa ukitazama kwa makini yeye ambaye ameenda kijijini kwa lengo moja kuondoka na malengo mawili haikumpasa kulaumu kwasababu hakufanya mandalizi ya kutosha kujua tabia ya mwenza wake. Basi tuwe makini tusipende kurusha lawama kwa jambo lolote tukubali kuwajibika kutokana na makosa yanayotokana na maamuzi ambayo tumefanya. Tukumbuke shida zote zinatokana na sisi wenyewe. #zaman #tanzaniantiktok🇹🇿 #tiktok #profjay #nikusaidiaje