@blessing_fantastic: Ubora wake unamfanya atambulike kama mmoja wa makipa bora zaidi barani Afrika kwa sasa. Diarra ana sifa ya kisasa ya kuwa Sweeper-Keeper, ana utulivu mkubwa anapokuwa na mpira miguuni na ana uwezo wa kuanzisha mashambulizi kwa usahihi wa hali ya juu akitokea nyuma, Pasi zake fupi kwa mabeki na mipira yake mirefu inayolenga washambuliaji imekuwa silaha kubwa ya kimbinu kwa timu yake. Kuna wakati amekuwa akionyesha hasira na jazba kali uwanjani, hasa pale timu yake inapofungwa goli au pale anapohisi waamuzi hawajatenda haki. Lakini sifa kubwa inayomtofautisha na makipa wengine ni ule uwezo wake wa kuzungumza na kuongoza safu yake ya ulinzi, Diarra anajua namna ya kuwapanga mabeki wake, kuamuru maeneo ya kukaa, na kuwapa ujasiri pindi wanapokabiliwa na washambuliaji hatari, hii inafanya ukuta wake kuwa mgumu kupenyeka. Ana ustadi wa Kuokoa Michomo, ana wepesi wa mwili na uwezo mkubwa wa kujipanga langoni, Mara kwa mara amekuwa akiibeba Yanga na Timu ya Taifa ya Mali kwenye mechi kubwa kwa kuokoa mashambulizi ya hatari ya ndani na nje ya kisanduku. Ana ukomavu wa hali ya juu na hana MAWENGE hata timu inapokuwa kwenye presha kubwa, anajua namna ya kusoma mchezo, kudhibiti kasi ya mechi, ana mbinu nyingi hata kuchelewesha muda pale inapohitajika ili kuilinda timu yake. Hali hii imemfanya kuendelea kuaminika kama kipa chaguo la kwanza kwenye kikosi cha Mali, ambacho kimejaa wachezaji wanaocheza soka la kulipwa barani Ulaya. Kutokana na viwango hivi, anatajwa kama kipa asiye na mpinzani wa karibu kwa sasa kwenye Ligi Kuu ya NBC nchini Tanzania: #viralvideo #yangasc #sports
Blessing Fantastic
Region: TZ
Thursday 24 September 2026 08:26:15 GMT
Music
Download
Comments
sabra mussa97 :
hakuna kama yanga kipa bora ni DIARA wetu tunampenda sanaaaa
2026-09-24 14:55:48
26
Rukia luckya :
Kuna huyu afu Kuna Aziz k Hawa watu wanaipenda San yanga 💚💛
2026-09-25 10:36:35
20
J. kimmich :
Namba Liwa One Goalkeeper bongo DJigui Diarra
2026-11-05 12:41:21
2
Rama :
tumia melod hi kwa kila shujaa wa yanga ime pendeza na itakua utambulisho wako kila tukiskia hu mdundo tuna jua uyo ni allan
2026-09-25 06:33:30
9
Mama wa Baraka :
I love you DJIGUI DIARRA
2026-09-27 19:22:24
2
Arafati Arafati Official🏅 :
yani kama kuna bahati Yanga wamewahi kuipata basi ni kuwa na huyu kiumbe kwenye Tim yao 😅
2026-09-25 06:00:09
11
pretty Bips♥️ :
diara wetu huyo kipa la Dunia sio Africa 💚💛💚💛💛
2026-09-24 10:39:36
11
p@tty £ddo24 :
kipa la boli
2026-09-24 11:11:46
4
Boniphace William :
kama diarra angekua mwalimu basi wanafunzi wangekua na kazi ya kufanya maan so kwa uwo ukali
2026-09-24 18:07:34
3
hamza shabani :
nzee.wakuwapangilia
2026-09-26 11:28:05
3
Charz p :
ajengewe sanamu huyu mwamba 💪💪💚
2026-09-24 16:19:09
5
MWAJABU KP :
jembe ni jembe tu wanazidi kukupa nguvu ya kuendelea kupata nguvu
2026-09-24 14:42:04
3
🫣🫵🏿 CHOTI ⛑️🇹🇿🪙💵 :
nampemda.shana diarra🎃😱😱😱😱
2026-09-25 14:23:59
1
johnwhite927 :
Kipa letuu hilooo wananchi.🔥💪
2026-09-24 20:18:09
2
Michael Fernandes :
Safi sana my braza 🥰🥰🥰
2026-09-25 05:59:43
1
_mili.tao :
Kuna mwaka mmoja walijaribu kusema Pinpin camara😂 ni bora kuliko Diara.. and debate is over😂
2026-09-27 07:43:35
1
Warda Raiton :
wow diarra 💛💚💛💚💛💚💛💚💛💚💛
2026-09-24 15:10:21
2
bamkari :
2026-09-25 05:41:23
1
kide :
yan uy kip ni atal
2026-10-21 14:52:09
0
Winnie Malisa🌸🐵 :
Likipa letu hilooo Dadekiii😂😂😂🔥🔥🔥
2026-11-11 07:57:38
0
pretty girl :
akihama yanga diarra tumeumia
2026-10-31 20:51:27
0
ju-lie🌸 :
kwenye kuchelewesha muda me huwa ananifurahisha aiseee......apewe maua yake jaman, he is the best keeper❤️
2026-10-22 09:44:33
0
ester💯💞 :
mmubeba lawama daah skuiz naona amepoa mm bnafs namiss hv vitu jmn
2026-11-04 21:38:51
0
Gerodi Mahundi :
respect my brother
2026-09-24 18:12:22
0
To see more videos from user @blessing_fantastic, please go to the Tikwm
homepage.