@jambotv_: VIDEO: Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Aridhini (LATRA) imesema itaendelea kuishauri Serikali kuhusu uwekezaji wa kampuni za mabasi katika eneo la Shekilango, ili kuhakikisha wawekezaji wanaotoa huduma kwa wasafiri hawaathiriki na changamoto zinazoweza kuvunja moyo wa kuendelea kuwekeza katika sekta ya usafiri. Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, CPA. Dkt. Habibu Suluo, amesema baadhi ya wawekezaji wamewekeza kwa kiasi kikubwa katika vituo na huduma mbalimbali kwa ajili ya wasafiri, hivyo ni muhimu kusikiliza changamoto zao na kuona namna ya kulinda uwekezaji wenye ufanisi. Amesema hayo wakati wa mkutano kati ya LATRA na wahariri wa vyombo vya habari, leo Septemba 24, 2026 akieleza kuwa LATRA itaendelea kuwa sehemu ya kuishauri Serikali kuhusu mazingira ya uwekezaji katika sekta ya usafiri, ili wawekezaji wasivunjike moyo na huduma bora kwa wasafiri ziendelee kupatikana.

Jambo TV
Jambo TV
Open In TikTok:
Region: TZ
Thursday 24 September 2026 16:15:56 GMT
19969
524
25
28

Music

Download

Comments

7u73s
7u73s :
Very SMART
2026-09-25 12:38:53
0
emanuelshashi
shashi manuel :
Professionalism yes Sasa No
2026-09-24 19:11:45
0
samairah.ahmed
Samairah Ahmed :
safi kabsaa warudishwe ss abilia tunapata shida sana maana tukipandia gari shekilango sk zote lazima ipitie stend ya magufuli ili ianze safari inangia na wanalipa ushuru ndyo tunaanza safari sasa shida Iko wapi
2026-09-24 18:32:37
4
jacksonmmbando5
jacksonmmbando855 :
hapana mbez Kwanza mengine baadae
2026-09-25 11:19:04
0
barton_leo95
Barton_Leo95 :
No Huwezi kuwa na stendi za mabus kila kona
2026-09-25 07:01:44
0
user1583520725848
Mercedes-Benz Ujerumani :
hamna poit hapo dunia nzima stand zinasehemu maalumu hasa mabasi kama haya yanayotokea kila mahali kwausalama wa nchi huwezi kuwaruhusu Kila mtu anajishushia Kila mahali lazima wapite sehemu moja maalumu acha kuwabembeleza wafuate sheria mkuu wa mkoa5 tena.
2026-09-25 04:48:26
0
kimidii3
mohamed kimidii :
mzee unaongea point ssna
2026-09-24 21:27:34
2
hisam.shaaban
Hisam Shaaban :
nimekuelewa kwa asilimia 100 ulo vizuri
2026-09-24 18:54:21
1
philbethlema1
philbethlema :
point
2026-09-25 04:40:03
0
kristin.sanka
Kristin Sanka :
unaongea baada ya watu kupata hasara
2026-09-25 16:00:42
0
adiam_collection
❤️ :
mwanza pia
2026-09-25 07:55:32
0
makuyunifinest.tz0
MAKUYUNI FINEST :
2026-09-24 23:37:32
0
abui_saratan
Abui_Saratan :
safi sana kiongozi.umeongea maneno machache sana lkn maneno yako yana akili sana.kula izo👉100%
2026-09-24 19:10:13
0
jumanneally661
Jumanne Ally :
Well said mkuu kweli Latra inajivunia wewe
2026-09-24 20:06:49
1
hamisi3204
hamisi :
kwani chalamila anashauriwa nanani kuropoka ropoka tumemchoka hapa dar
2026-09-25 12:20:18
0
veilamremi0
veilamremi :
jamani kama wanafunzi wanapata shida na stendi ni fujo na wenye mabasi wanatafuta Abiria aoni basi ni kero
2026-09-25 14:30:26
0
harunasulley34
Haruna sulley🇹🇿 :
Kiko wapi chamalila????
2026-09-25 06:40:42
0
fashi203
A-FASHION :
🤝🤝🤝🤝🤝🤝🤝🤝🤝🤝🤝
2026-09-25 08:21:34
0
To see more videos from user @jambotv_, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About