@sasibuying_area: OnePlus ilianza 2013 ikiwa na wazo moja tu: Flagship Killer—simu zenye uwezo wa juu zaidi kwa bei ya chini. Kutoka kwenye mtindo wao wa zamani wa kuuza kwa alama ya "Invite Only" na mfumo wa OxygenOS uliopendwa na wengi, hadi leo kuwa miongoni mwa majitu kwenye soko la flagship na foldable. Licha ya kubadilika sana kwa miaka na kuingia zaidi kwenye mfumo wa mainstream, kauli mbiu yao bado inabaki pale pale: Never Settle. ⚡📱 Unakumbuka simu gani ya OnePlus iliyowahi kukunogesha zaidi au unayotumia mpaka leo? #oneplus #neversettle #techupdates #flagshipkiller