@openonlinemedia: Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imefanya marekebisho ya ratiba ya upimaji na mitihani ya Taifa kwa mwaka 2026, kufuatia uwezekano wa kutokea kwa mvua kubwa zinazohusishwa na hali ya hewa ya El Nino katika maeneo mbalimbali nchini. Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Septemba 25, 2026, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Wanu Hafidh Ameir, amesema hatua hiyo imechukuliwa baada ya Serikali kufuatilia kwa karibu taarifa za hali ya hewa na kutathmini athari zinazoweza kujitokeza katika uendeshaji wa mitihani ya Taifa. Amesema kwa mujibu wa utabiri rasmi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, TMA, kuna uwezekano wa kutokea El Nino yenye nguvu, huku mvua zikitarajiwa kuanza katika baadhi ya maeneo mwezi Oktoba na kuongezeka zaidi mwezi Novemba 2026. Ameeleza kuwa hali hiyo inaweza kuathiri usafiri wa wanafunzi, walimu, wasimamizi na maafisa wa mitihani, pamoja na kufikika kwa baadhi ya vituo vya mitihani, hivyo Wizara kwa kushirikiana na Baraza la Mitihani la Tanzania imefanya marekebisho ya ratiba ili kupunguza changamoto hizo. Kwa mujibu wa ratiba iliyorekebishwa, Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Pili Ngazi ya Shule utafanyika Oktoba 7 na 8, 2026, wakati Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne utafanyika Oktoba 5 na 6, 2026. Aidha, Upimaji wa Kitaifa wa Kidato cha Pili utafanyika kuanzia Oktoba 12 hadi 23, 2026, huku Mitihani ya Kidato cha Nne ikianza Oktoba 19 hadi Novemba 6, 2026. Marekebisho hayo yanalenga kuhakikisha wanafunzi wanafanya mitihani katika mazingira salama na yenye utulivu. Naibu Waziri amesema Serikali itaendelea kufuatilia mwenendo wa hali ya hewa na kuchukua hatua stahiki kwa kushirikiana na mamlaka na taasisi husika, ili kuhakikisha upimaji na mitihani ya Taifa inafanyika kwa utaratibu unaofaa, huku usalama wa wanafunzi, walimu, wasimamizi na wadau wengine ukipewa kipaumbele. #Pakua App ya #OpenMedia playstore kusikiliza #DoubleORadio na kutazama #OpenMTV au kupitia tovuti #openmedia.co.tz, Kwa Matukio, Habari na Matangazo wasiliana nasi 0677107271 au 0677107273.
Open Online Media
Region: TZ
Friday 25 September 2026 11:52:16 GMT
Music
Download
Comments
shebby @2005 :
aàaah ki2 roho inapenda jamn nishachok Mimi man hawa academic jau san
2026-09-25 20:08:20
0
🎁💝Bella💖💍💗 :
mmmmh MUNGU naamini hakuna alumino.
2026-09-25 14:44:59
9
Dada mzurii :
EMUNGU TUSAIDIE BILA WEWE HATUWEZI KITU SIMAMA BABAH
2026-09-25 14:27:13
6
onesmoemmanuel36 :
hakuna elimino nakataaa kwa jina la.YESU kwa kumanisha
2026-09-25 19:58:07
3
leonia :
Mungu simamia mitiani yetu
2026-09-25 17:39:09
5
karu :
kwakweli kama ni mchongo mmeupanga kwa ustadi.
2026-09-25 15:03:02
4
Da 2 :
mmmh tuna gund 4m four wa mwaka huu darasa 4/2019 tulipata coran darasa 7/2022 tulipata sensa mwaka huu mvua 🙏🙏🙏
2026-09-25 18:14:21
3
flowerbeut girl🥰🥰 :
Ni mitihani ipi mnayosema? ni ya kidato cha 4 ama shule za msingi? tafadhali nielewesheni kwa anayeelewa
2026-09-25 17:08:21
3
mahra😍 :
MUNGU wetu tunaomba utuepushie hili🙏🙏
2026-09-25 14:31:24
3
TrendVerse :
mitihan yote ya TAifa mwaka huuu ratiba
2026-09-25 17:33:40
2
WISDOM :
namshukulu mungu siaminikama namaliza shule kidato Cha mtihan[Red heart] mungu tusaidie watoto wako tunaofanya mtihan natujalie tutakapo Fanya mtihan tufaulu site mtihan adiferi hata mtu mmoja jaman itaniuma
2026-09-25 18:12:23
2
baby face cp :
aise achen watoto bc
2026-09-25 14:53:22
2
Khayriya Salim :
ALLAH ATUHIFADHI WAJA WAKE YA RABB IWE SALAMA
2026-09-25 15:10:38
4
JitaMan :
hiyo mvua iponyesha mtatuambia nn
2026-09-25 13:51:17
2
🎀baby🎀cute :
mung atusimamiy
2026-09-25 21:02:12
0
Fatuma Namoto :
tusome jaman tuson
2026-09-25 19:57:58
0
OFFICIAL CRAZY💥💥 :
waje 2 mtaani kazi ni nyingi
2026-09-25 20:11:07
0
Kulthum1976 :
ovyo unamkata naibu waziri badala kuacha watu wakajua tarehe ovyooo
2026-09-25 18:53:19
0
Mwajuma Omari :
Mungu tunusuru waja wako
2026-09-25 18:37:20
0
habibahinda8 :
mungu saidia ufaham wetu , kazi ya walim wetu na shule yetu
2026-09-25 21:43:59
0
ispectol maladhi :
🥰🥰🥰
2026-09-25 20:16:44
0
ISSA :
🥺🥺🥺🥺🥺
2026-09-25 18:50:39
0
JOEL MUSSA :
🥰🥰🥰
2026-09-25 17:48:56
0
Sefrose Missan :
😳😳😳
2026-09-25 16:51:01
0
anjero :
😳😳😳
2026-09-25 20:42:55
0
To see more videos from user @openonlinemedia, please go to the Tikwm
homepage.