@afya.ya.mama.na.mtoto.tz: Kama unataka kuongeza uzito kwa njia yenye lishe, si kula matunda tu bali kuyachanganya na vyakula vingine vyenye nishati, protini na mafuta yenye afya. 🍌 Matunda yanayoweza kusaidia kuongeza uzito. 1. Parachichi 🥑 Ni miongoni mwa matunda yenye mafuta mazuri na calories nyingi. Linaweza kusaidia kuongeza energy intake, hasa likichanganywa na vyakula vingine. 2. Ndizi 🍌 Zina wanga na calories, hivyo ni rahisi kuongeza kwenye mlo. Unaweza kula pamoja na oats, karanga au mtindi. 3. Tende 🌴 Zina sukari ya asili na calories nyingi kwa kiasi kidogo, hivyo zinaweza kuwa snack nzuri kwa mtu anayehitaji kuongeza calories. 4. Nazi 🥥 Maziwa ya nazi na nyama ya nazi vina mafuta na energy nyingi. Vitumie kwa kiasi ndani ya mlo. 5. Embe 🥭 Lina carbohydrates na calories, na pia hutoa vitamini mbalimbali. Ni rahisi kutumia kama snack au sehemu ya smoothie. 6. Zabibu 🍇 Zina carbohydrates na natural sugars, na zinaweza kuongeza calories kwenye mlo bila kushiba sana. 💡 Siri kubwa ya kuongeza uzito Matunda pekee hayatoshi. Tengeneza mlo wenye matunda + protini + wanga + mafuta yenye afya. Mfano: ndizi + oats + maziwa/mtindi + karanga Unataka kuongeza uzito kwa afya? Anza kuangalia ubora na kiasi cha chakula unachokula kila siku, si kushiba tu. #AfyaBora #UngaWaLishe #LisheBora #KuongezaUzito #LisheYaMtoto
Emmy_Lishe_tz.
Region: TZ
Friday 25 September 2026 12:31:30 GMT
Music
Download
Comments
Iron butterfly 🦋 :
tende unatumiaje
2026-10-07 17:06:25
1
To see more videos from user @afya.ya.mama.na.mtoto.tz, please go to the Tikwm
homepage.