@katorotv: Mkuu wa Mkoa wa Geita, Alexander Mnyeti, ameliagiza Jeshi la Polisi mkoani humo kuendelea kuwakamata madereva wa bodaboda wanaokiuka sheria za usalama barabarani, akisema hatua hiyo ni muhimu kudhibiti ajali na kulinda usalama wa wananchi. Akizungumza katika mkutano wa viongozi na wananchi uliofanyika Katoro mapema Septemba 24, 2026, Mnyeti alisema polisi wanapaswa kuwachukulia hatua bodaboda wanaopita kwenye taa nyekundu, wasiovaa helmeti na wanaofanya vitendo hatarishi barabarani, huku akisisitiza kuwa madereva wanaofuata sheria hawapaswi kusumbuliwa. Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa alisema baadhi ya bodaboda wamekuwa wakifika kwa wingi kumtetea mwenzao anapochukuliwa hatua, akionya kuwa tabia hiyo haipaswi kuendelea. Mnyeti alisisitiza kuwa udhibiti huo si wa kuwaadhibu bodaboda wote, bali ni kuhakikisha wanaokiuka sheria wanawajibishwa, huku wanaofuata sheria wakifanya kazi zao bila usumbufu.
KATORO TV
Region: TZ
Friday 25 September 2026 13:05:52 GMT
Music
Download
Comments
Bonge La bwana :
asa unamwambia Nani izo habr zako
2026-09-25 20:50:15
0
Bahati Homango figherman :
kwenye kampen bodaboda tunaitwa maafisa usafirishaji na sio bodaboda
2026-09-25 21:02:11
2
Naisho Tossy :
hii nchi kila mtu beberu sasa hatujui tumsikilize nani😳😳😳
2026-09-25 19:09:25
5
stephen_gamaya :
president 20230
2026-09-25 15:38:00
1
Ley :
wazir mkuu amesema boda boda asikamatwe we unasema kamata
2026-09-25 15:04:48
9
tayoboi m a t e y :
waziri mkuu katoa tamko... mkuu wa mkoa katoa tamko.. sheria ya usalama barabarani nayo inatoa tamko.. NGOJA tusikilizie tamko lingine
2026-09-25 15:38:27
8
Nyang'ombe :
huyu ndo Mnyeti ni kweli kiongoz
2026-09-25 14:42:49
12
J BENDERA 🇹🇿 :
kwenye kapeni boda boda fresh
2026-09-25 19:12:03
5
Tz🇹🇿 :
asa hapo geita kna taa jaman
2026-09-25 18:46:57
3
Tabarak Rahman :
UONGO tuuu
2026-09-25 19:15:35
2
1dickson01 :
Wameshaniuz Siwez kufata Sheria
2026-09-25 17:27:36
1
Pinishi Kikoti :
kwenye ajari mheshimiwa sio kweli
2026-09-25 17:47:06
1
The rider🏍️🏍️ :
kwani uchaguzi ni lini????
2026-09-25 18:51:41
2
Hans Ernest :
japo hao jamaa wana nguvu mheshimiwa wakikuchukia kaz yako itakuwa ngum sana kiukweli kabisa boda kuna wakati tunanzingua
2026-09-25 15:29:07
5
user14967881935062 :
nikwer
2026-09-25 14:22:21
2
Hassan kileo :
uchaguzi upo mbali 🤣🤣🤣
2026-09-25 18:44:51
1
King mtoto 🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿💖 :
hii inchi watu wanapenda kujiamlia mambo ila bc tu 🥱🥱🥱🥱🥱🥱
2026-09-25 18:23:24
3
edwardsilas :
sisi tupo na waziri mkuu baba yetuu mtetez wetu
2026-09-25 19:03:10
1
tumain anathory kilomba :
sasa nashindwa kuelewa tumusikilize nan kati ya wazir mkuu na mkuu wa mkoa
2026-09-25 20:45:17
0
zephania :
Waziri mkuu katoa agizo jingine mkuu wa mkoa nae kaja na jingine nani tumuelewe sasa jaman nachoka mieeeee
2026-09-25 19:24:21
0
Hassan matelephone :
Kuna vingi vya kusema au kufanya sio kuwaonea bodaboda
2026-09-25 19:12:35
1
Victor Wilbard Mlaki :
kazi na utu
2026-09-25 18:32:34
1
AMOS✅️✅️⭐️⭐️ :
sasa api kosa nilipi bodaboda mbona tuna andamwa ivi
2026-09-25 17:54:25
2
kakabeka OG :
..ukweli ni kwamba boda hawafati Sheria
2026-09-25 16:27:20
1
yori yori_197 :
Bodaboda tatizo kubwa mnoo hapa nchini hawafuati sheria hawavai helment pikipiki zao asilimia kubwa hazina bima wanapakiza watu zaidi ya wawili mpaka watano. Wengine wanazibua ecssos za pikipiki zao ili zipige kelele wanapita mitaaani usiku watoto wachanga wanaamka wazee na wagonjwa wenye presha wanateseka. Yani kama hakuna sheria
2026-09-25 16:29:49
2
To see more videos from user @katorotv, please go to the Tikwm
homepage.