@sdatanzania: Sabato Njema! 🕊️🤍 Sabato imetufikia tena ikiwa ni zawadi ya Mungu ya muda wa kutulia, kumwabudu Muumba wetu na kurejesha nguvu za kiroho kwa kuweka Mahusiano tena na Muumba! Katika pilikapilika za maisha, Mungu anatualika kuweka kando shughuli za kawaida na kuelekeza mioyo yetu kwake. Ni wakati wa kusoma Neno lake, kuomba, kushirikiana na waamini wenzetu na kutafakari wema wake katika maisha yetu. Tunawatakia washiriki na Waumini wote wa Kanisa la Waadventista Wasabato Sabato yenye amani, ibada yenye baraka na uwepo wa Mungu katika kila hatua. Sabato Njema na yenye baraka. Mungu awabariki. 🙏🏽 #SDATanzania #SabbathBlessings #SabbathMessage #creatorsearchinsights #7thdayadventist