@nattahpipoh_: Meja Jenerali Jackson Jaelous Mwaseba alizaliwa mnamo Tarehe 21 Aprili, 1967 katika Kijiji cha Lugombo, Kata ya Mwaya, Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya. Alianza safari yake ya kisomo katika Shule ya Msingi Mwaya (1975–1981) kabla ya kujiunga na masomo ya sekondari katika Shule za Mbalizi na Mburu kati ya Mwaka 1982 na 1985. Akiwa na kiu ya elimu ya juu, Meja Jenerali Jackson Mwaseba alijiunga na Shule ya Sekondari ya Mzumbe (A-Level) Mkoani Morogoro kwa masomo ya Kidato cha Tano na Sita (1986–1988). Baada ya kuhitimu Mzumbe, alipitia mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) katika kambi za JKT-Oljoro na Makuyuni mkoani Arusha (1988–1989) hatua hiyo ilimwekea Msingi thabiti wa uzalendo na nidhamu ya kijeshi ndani ya moyo wake. Meja Jenerali Jackson Mwaseba, Alipohitimu Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na kutunukiwa Shahada ya Kwanza ya Elimu (Bachelor of Arts with Education) mwaka 1993. Hakukomea hapo aliendelea na masomo ya uzamili pale pale UDSM na kutunukiwa Shahada ya Uzamili ya Lugha (Master of Arts in Linguistics) mnamo mwaka 1996. Mnamo Tarehe 19 Februari, 1997, Meja Jenerali Jackson Jaelos Mwaseba alijiunga rasmi na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ). Baada ya kufuzu mafunzo ya Maafisa Wanafunzi, alitunukiwa Kamisheni ya Uafisa katika cheo cha Sub-Lieutenant (Luteni Usu) mnamo Tarehe 2 Mei, 1998. Ili kujiimarisha kimbinu na kiuongozi, Meja Jenerali Jackson Jaelos Mwaseba alihudhuria kozi na mafunzo mbalimbali mazito ya kijeshi: Mafunzo ya Uongozi wa Platoon na Kampuni (Tanzania, 2000–2001), Kozi ya Makamanda na Unadhimu (Tanzania, 2003), High Commander Defence Studies (Tanzania, 2009), War College Course (Marekani, 2010) Hapa alipata Shahada ya Pili ya Uzamili katika Mkakati wa Kijeshi (Master’s Degree in Strategic Studies). Kutokana na nidhamu, Uchapakazi na uwezo wake wa hali ya juu wa uongozi ulimfanya apande vyeo kwa ufanisi mkubwa ndani ya JWTZ kutoka kuwa Luteni (1998) hadi Meja Jenerali (2024). 1. Luteni. 2 Mei 1998 2. Kapteni. 3 Machi 1999 3. Meja. 29 Januari 2001 4. Luteni Kanali. 11 Januari 2007 5. Kanali. 6 Oktoba 2009 6. Brigedia Jenerali. 12 Aprili 2018 7. Meja Jenerali. 21 Julai 2024 Katika utumishi wake, Meja Jenerali Jackson Jaelos Mwaseba amekuwa nguzo muhimu katika Taaluma, Udiplomasia wa kijeshi na mafunzo ya Maofisa. Amehudumu kama Mkuu wa Taaluma na baadaye Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Makongo (2001–2009), Mkufunzi na Mwelekezi katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) na Msaidizi wa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi (2012–2014). Utumishi wake ulimvusha mipaka ya nchi hadi jijini London, Uingereza, ambapo alihudumu kama Mwambata wa Jeshi (Military Attaché) kuanzia mwaka 2014 hadi 2020. Baada ya kurejea nchini na kuhudumu kwa muda kama Kaimu Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC), aliteuliwa kuwa Mkuu wa Chuo cha Maafisa Wanafunzi Monduli (TMA-Monduli) mwaka 2020, Chuo hiki cha kimkakati kinachochonga na kuandaa viongozi wa baadaye wa Jeshi la Tanzania. Kutokana na mchango wake uliotukuka katika ulinzi wa Taifa, Operesheni za kimataifa na uaminifu wa hali ya juu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amir Jeshi Mkuu, amemtunuku nishani mbalimbali za heshima: 1. Nishani ya Miaka 40 ya JWTZ. 2. Nishani ya Operesheni Demokrasia Comoro. 3. Nishani ya Utumishi Mrefu. 4. Nishani ya Miaka 50 ya Uhuru. 5. Nishani ya Miaka 50 ya JWTZ. 6. Nishani ya Miaka 60 ya Uhuru. 7. Nishani ya Utumishi Uliotukuka. 8. Nishani ya Kumbukumbu ya Muungano Daraja la Nne. 9. Nishani ya Miaka 60 ya JWTZ Major General Jackson Jaelos Mwaseba anabaki kuwa mfano wa kuigwa wa Jinsi elimu, Nidhamu na Ujasiri vinavyoweza kumvusha mwanadamu kutoka maisha duni ya kijijini hadi kuwa mmoja wa viongozi waandamizi na wakuheshimika kabisa katika Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania na secta nyingine. kyela.. #mbeyatikitok🇹🇿🇹🇿 #tanzaniatiktok🇹🇿🇹🇿❣️🇰🇪🇰🇪♥️ #fyppppppppppppppppppppppp #kyelambeyatanzania #kyelambeyatanzania @NATURE OF KYELA🥷✍️ @Nattahpipo_SPORTS WEAR STORE🏅 @lugerRb@099 @𝐍 𝐀 𝐌 𝐒 𝐇 Į 𝐍 3 8
Nattahpipoh_kajubili🦍
Region: TZ
Saturday 26 September 2026 09:08:08 GMT
Music
Download
Comments
mwakipesilebrown :
mwaseba🫡
2026-09-26 15:57:08
0
Dr. Simon :
Tuliosoma makongo secondary tujuane
2026-09-26 16:20:10
2
Wavoda :
Mungu amuongoze vema mzee wetu ampe afya njema kwakweli tuzidi kumuombea wanakyela.
2026-09-26 11:12:05
2
1235🇹🇿 :
one good thing if not two,,mzee hazeeki, mtu poa sana
2026-09-27 13:34:27
0
Eng. Amos :
ni Jairos sio Jaelos
2026-09-27 15:37:33
0
g@petrouswege1995 :
kyela tumetoka viongozi wenginwa kijeshi akiwemo msaafu mwamunyange
2026-09-27 07:35:30
0
am14578 :
CV yake ni ya mambo ya utawala zaidi wa maofisini sio ya kivita au kuongoza brigade za vikosi vya kivita viwe vya anga ,ardhini au angani au hata kuwa kamanda wa kikosi kimojawapo cha vita
Yuko kiofisi zaidi sio maeneo ya kivita
2026-09-27 13:05:37
0
👁 :
afya njema mzee wetu
2026-09-27 04:27:25
0
Martha♥️♥️♥️ :
nsloli Jo jujujo
2026-09-26 18:18:44
1
Roby Emanwel :
jila la hu wimbo
2026-09-26 13:22:21
0
1235🇹🇿 :
2001 hadi 2009 hakuwa mkuu wa shule ya makongo,
2026-09-27 13:32:52
0
Swagg 🐕 vibez :
uyu wandondaghaaa😂
2026-09-26 14:31:04
0
Usdollar@1999. :
mm ni mtu wa Kyela jamani,kwani huyu mzee wetu,ndoo amekuwa mkuu wa majeshi au kwa sasa ana cheo gani? maana CV yake naiona imeshiba sana
2026-09-26 16:46:28
1
Tz sweetmelanin22🌚🧚🏿♀️ :
@🎻..RENEEZ 🤎
2026-09-26 18:48:48
1
@sprinter🦋 :
🪖🫡🫂
2026-09-26 16:11:05
0
To see more videos from user @nattahpipoh_, please go to the Tikwm
homepage.