@udhaifa.swalehe: Siku moja, Sayyidna Musa (A.S.) alifunga safari kuelekea Mlima Sinai, kwa ajili ya kwenda kuzungumza na Mwenyezi Mungu. Akiwa njiani, alikutana na mtu mmoja miongoni mwa Wana wa Israili. Yule mtu alimsalimia Nabii Musa (A.S.), kisha akamuuliza: Ewe Nabii wa Mwenyezi Mungu, unaelekea wapi? Nabii Musa (A.S.) akamjibu: Ninaelekea kuzungumza na Mwenyezi Mungu. Yule mtu akasema: Sawa. Lakini nitakapokuomba, ukifika huko tafadhali nisaidie kumwambia Mwenyezi Mungu jambo moja. Mimi amenipa mali nyingi sana mpaka nimezidiwa nazo. Naomba aniwezeshe kuwa na mali kidogo. Nabii Musa (A.S.) akamjibu: Sawa, nitamfikishia ujumbe wako. Akaendelea na safari yake. Baada ya muda, njiani akakutana na mtu mwingine aliyekuwa maskini sana. Alikuwa akiishi katika nyumba duni na hali yake ilikuwa ngumu. Yule mtu naye alipomuona Nabii Musa (A.S.) akamuuliza: Ewe Nabii wa Mwenyezi Mungu, unaelekea wapi? Nabii Musa (A.S.) akamjibu: Ninaelekea kuzungumza na Mwenyezi Mungu. Yule maskini akasema: Basi, tafadhali ukifika huko, mwambie Mwenyezi Mungu: Mbona hanikumbuki? Mbona ameniacha katika hali hii ya ufukara? Kwa nini hanipi mali na maisha mazuri? Nabii Musa (A.S.) akamjibu: Sawa, nitamfikishia ujumbe wako. Akaendelea na safari mpaka akafika Mlima Sinai. Alipofika, Nabii Musa (A.S.) akamueleza Mwenyezi Mungu kuhusu watu wale wawili. Akasema: Ewe Mola wangu, nimekutana na mja wako mmoja ambaye umempa mali nyingi sana. Anaomba umsemeshe na umupunguzie mali hiyo. Na mwingine ni maskini anayesema kwamba kwa nini humkumbuki na kwa nini umemwacha katika hali ya ufukara. Mwenyezi Mungu akamwambia Nabii Musa (A.S.): Ewe Musa, nenda ukamwambie yule mwenye mali nyingi: Ikiwa anataka mali yake ipungue, basi anikufuru Mimi. Kisha kuhusu yule maskini, akaambiwa: Mwambie: Ikiwa anataka kuongezewa neema, basi kwanza anishukuru kwa hali hiyo aliyonayo. Nabii Musa (A.S.) akarudi kutoka katika safari yake. Kwanza akaenda kwa yule mtu tajiri na kumfikishia ujumbe wa Mwenyezi Mungu: Mwenyezi Mungu amesema: Ikiwa unataka mali yako ipungue, basi nikufuru Mimi. Yule mtu aliposikia maneno hayo, akashtuka sana. Wakati huo alikuwa ameshika glasi ya maji mkononi. Kwa mshangao, glasi ile ikamdondoka. Akasema: Hapana! Mimi siwezi kabisa kumkufuru Mola wangu! Kila nilicho nacho ni neema kutoka Kwake. Na hapo, kwa mujibu wa simulizi hili, kile kilichokuwa mkononi mwake kikabadilika na kuwa dhahabu. Yule mtu akazidi kumshukuru Mwenyezi Mungu na akatambua kwamba mali yote aliyopewa ilikuwa ni neema kutoka kwa Allah. Baada ya hapo, Nabii Musa (A.S.) akaendelea mpaka akamfikia yule maskini. Akamwambia: Mwenyezi Mungu amesema: Ikiwa unataka kuongezewa mali na neema, basi kwanza mshukuru kwa hali uliyonayo. Yule maskini akastaajabu na kusema: Ewe Musa! Kweli nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa hali hii ya ufukara niliyonayo? Kwa kweli, mimi sioni kitu cha kushukuru katika maisha yangu haya. Na katika simulizi hili, mara upepo mkali ukavuma na kuliondoa paa la nyumba yake pamoja na lile shuka alilokuwa amejifunika. Akaachwa bila nyumba na bila shuka. Hapo ndipo alipoanza kujilaumu na kutambua kwamba hata nyumba yake duni na lile shuka alilokuwa akiliona kuwa si kitu, vilikuwa ni neema kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Akatambua kwamba mwanadamu wakati mwingine huona neema alizonazo kuwa ni ndogo, mpaka pale zinapomwondokea ndipo anapotambua thamani yake. MAFUNZO Kisa hiki kinatukumbusha kwamba tusimdharau Mwenyezi Mungu kwa sababu ya neema ndogo tulizonazo. Huenda kile tunachokiona kuwa ni kidogo, kwa mwingine ni ndoto kubwa. Nyumba uliyonayo inaweza kuwa ndogo, lakini ni neema. Nguo uliyonayo inaweza kuwa ya kawaida, lakini ni neema. Afya uliyonayo ni neema. Chakula unachokula ni neema. Familia uliyonayo ni neema. Na hata pumzi unayovuta kila siku ni neema kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo, tusisubiri mpaka neema ituondokee ndipo tutambue thamani yake. Mwenyezi Mungu atujalie kuwa miongoni mwa waja Wake wenye kumshukuru katika kila hali tunayopitia. Aamiin.š¤².
Abuu salmaniš
Region: TZ
Saturday 26 September 2026 10:57:07 GMT
Music
Download
Comments
@minnie :
Ameeen
2026-09-26 13:04:49
0
aisha azali :
amiiin
2026-09-26 12:30:54
0
Abdur :
amiina
2026-09-26 11:49:46
0
momš„° :
šš„°
2026-09-26 13:20:10
0
To see more videos from user @udhaifa.swalehe, please go to the Tikwm
homepage.