Sqndag Acrey :
Verse: Sasa naingia booth, naingia na pressure ya kizazi, Kila line ni testimony, siyo story za kubuni mezani. Nimeona dreams zikifa kwa sababu mfuko hauna hela, Nimeona vipaji vikizikwa kwa sababu connection imekataa.
Lakini still we move, hata njia ikiwa rough, Mtaa umetufanya tough, lakini mioyo bado soft. Hatuna laana, tunatafuta nafasi tu ya kupumua, Tukipata mic, tunasema yaliyofichwa na wenye nguvu. Wengine wanataka flex, sisi tunatafuta survival, Wao wanaongea kwa Wi-Fi, sisi tunapanga kwa signal. Kihuni kabisa, nikibanwa natoa meno kama simba, Sio kwamba napenda vita, ila njaa ikifika inabadilisha lugha…….
2026-10-08 22:15:07