@mnec.ussi: TUSICHANGANYE SIASA NA UHAI WA WANANCHI Mbunge wa Jimbo la Malindi, Mhe. Muhsin Ussi, amewaomba wananchi wa Mji Mkongwe kuunga mkono hatua za Serikali za kuwahamisha wananchi wanaoishi katika makaazi hatarishi, hususan katika kipindi cha mvua za El Niño. Aidha, amewataka wanasiasa kutotumia changamoto za wananchi kama fursa ya kujijengea umaarufu wa kisiasa, akisisitiza kuwa usalama na uhai wa wananchi vinapaswa kuwa mbele ya maslahi ya kisiasa. Mhe. Muhsin ameyasema hayo katika mkutano maalum na wananchi wa Mji Mkongwe uliofanyika Skuli ya Hamamni, uliolenga kutoa elimu na tahadhari kuhusu mvua za El Niño zinazotarajiwa kuanza mapema mwezi Oktoba.