@madininews: Moto mwingine mteketeza nyika umezuka alfajiri ya leo Jumatatu katika Mlima Kilimanjaro, ukisambaa kutoka eneo la Sangarini karibu na mwinuko wa Kamwanga kuelekea Shira Plateau upande wa magharibi wa mlima huo. Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) imethibitisha kuwa tayari timu ya wazima moto, maafisa wa uhifadhi, wadau wa utalii, na wananchi wamepelekwa eneo la tukio linalokadiriwa kuwa mita 3,800 kutoka usawa wa bahari ili kuudhibiti. Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi wa TANAPA, Catherine Mbena, ameeleza kuwa changamoto kubwa inayokabili juhudi hizo ni upepo mkali na uoto unaowaka kwa urahisi, huku akisisitiza kuwa chanzo bado hakijafahamika na kwamba shughuli za utalii na upandaji mlima zinaendelea kama kawaida bila kuathiriwa na janga hilo.

MADINI TV
MADINI TV
Open In TikTok:
Region: TZ
Monday 28 September 2026 09:02:35 GMT
3412
48
1
1

Music

Download

Comments

lazachris8
lazachris :
hamnaga walinzi hapo mlimani,hiyo ni vita ya kiuchumi asa wa utalii na majirani
2026-09-28 10:14:05
0
To see more videos from user @madininews, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About