@gillybonny_tv: Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Deogratius Ndejembi, amezitaka taasisi na mashirika ya umma kutumia nafasi walizonazo kuwaandaa vijana ili waweze kushindana katika soko la ajira nchini Tanzania, Afrika na duniani. Ndejembi ameyasema hayo wakati akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa kikao kazi cha wenyeviti wa bodi na watendaji wakuu wa taasisi na mashirika ya umma (C-CEOs Forum) 2026, kilichofanyika katika Ukumbi wa AICC Arusha. Amesema kuna changamoto kwa wahitimu wanaotakiwa kuwa na uzoefu wa miaka kadhaa kabla ya kupata ajira, akieleza kuwa taasisi za umma zina nafasi ya kuwapa vijana uzoefu na ujuzi unaohitajika. “Graduate anaambiwa lazima awe na uzoefu wa miaka mitatu, miaka mitano... uzoefu huo ataupata wapi? Kama sisi kwenye taasisi zetu za umma hatutotumia taasisi zetu katika kuwaandaa vijana hawa ili waweze kuwa na uwezo wa kushindana katika soko la ajira la Tanzania, Afrika Mashariki, Afrika na duniani kwa ujumla” Aidha, Ndejembi amesema licha ya vijana 3,200 kuandaliwa kuingia katika soko la ajira, juhudi hizo bado haziendani na kasi inayohitajika katika kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2050. Ameonya kuwa taasisi za umma zisipotumia nafasi walizonazo kuwaandaa vijana, taifa linaweza kupoteza nguvu kazi ya leo ambayo ni muhimu katika kufikia malengo ya maendeleo ya mwaka 2050.

Gilly Bonny Tv
Gilly Bonny Tv
Open In TikTok:
Region: TZ
Monday 28 September 2026 12:47:40 GMT
9398
323
16
22

Music

Download

Comments

haubatj
Elly prukit :
Best leader 🙌
2026-09-29 04:48:01
0
amosikulwa693
amosi kulwa :
hongera mheshimiwa asante kwa kutusemea
2026-09-28 19:53:59
2
odiliah_56
beatus mhagama :
asande kiongoz wetu
2026-09-29 03:38:56
0
user407181055477
user407181055477 :
asante mkuuu wetu
2026-09-28 16:44:32
1
abedi962
Abedi🧠 :
🔥🔥 ulikuwa wapi baba
2026-09-29 10:49:11
0
doctar12346
doctar1234@ :
mkuu mkuu haya maneno kuwa nao makini Baba CCM Baba hawataki maneno hayo Baba subir ushike kiti Baba Kwa sasa MDA bado
2026-09-29 13:21:23
0
shaban.wambura
SHABAN WAMBURA :
hongera sana mh.makamu wa rais
2026-09-28 20:15:21
0
kashyusedcartz
kashy649 :
🤣 🤣 🤣 🤣 Kama wanaelewa vile
2026-09-28 20:31:00
0
user39471598203784
flr :
Asante sana mheshiwa mm nipo tayar hata kesho kwenda kujitolea nilipwe iyo kiasi
2026-09-28 20:21:55
0
user11085920850862
madam Diana :
unakuja kuja
2026-09-28 20:13:41
0
ivyx_45
ivyx_45🫰 :
Akili Mkubwa
2026-09-28 14:44:52
1
user31011773686887
user31011773686887 :
kwa kweli mimi simsikilizaji hutba lakin kwa huyu makamu wa raisi kija mchapakazi naakiongea unatamani asimalize kuzungumza
2026-09-28 17:52:18
1
maryciana.sheka
Maryciana Sheka :
💯💯💯
2026-09-28 18:04:06
0
user9698581671982
Feferajani :
🥰🥰🥰
2026-09-28 20:18:26
0
To see more videos from user @gillybonny_tv, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About