@uhuruonline: #HABARI : MAKAMU wa Rais Deogratius Ndejembi, amezitaka Wizara ya Mipango na Uwekezaji, Fedha na Kilimo, ndani ya wiki mbili kuandaa mpango wa kuwawezesha vijana 10,000 kupata utaalamu na ujuzi utakaowaongezea tija katika shughuli za kiuchumi katika maeneo yao. Ndejembi amesema vijana hao wanapaswa kuwezeshwa kulingana na shughuli za kiuchumi zinazofanyika katika maeneo yao, ikiwemo kilimo cha korosho Mtwara, zabibu Dodoma na pamba katika maeneo yanayolima zao hilo. Amesema mpango huo utawasaidia vijana hao kupata ujuzi unaoendana na fursa zilizopo katika maeneo yao, hatua itakayowawezesha kujiajiri na kupata fursa za ajira. Ndejembi amesema ndani ya wiki mbili anatarajia kupokea mpango huo ili aweze kuwasilisha taarifa kwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na kuanza utekelezaji wa mpango huo. Ndejembi ametoa maelekezo hayo leo, Septemba 28, 2026, akimwakilisha Rais Dk. Samia katika Kikao cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa (AICC), jijini Arusha. #uhuruonline #uhuruupdates
uhuruonlinetz_
Region: TZ
Monday 28 September 2026 15:04:42 GMT
Music
Download
Comments
Saidi Mabula :
Jamaa ukimsikiliza bila makasiriko ana kitu
2026-09-28 17:18:19
63
AZORY J ZAKARIA :
huyu kweli ni kijana anaweza kulisaidia taifa
2026-09-28 17:43:56
27
wakilidumchelenj8 :
ccm bahna hawa jamaa wanajuwa kuandaa viongozi wao cheki huyu jamaa anavyopafom kwa umakini na utulivu na kimamlaka yaani utahisi anamiaka 20 kwenye nafasi hio
2026-09-28 19:14:25
21
pascalntunda :
This is perfect approach, Tutatengeneza skilled people
2026-09-28 18:52:26
7
geofreygadi :
unaongea vizur ila tuanze na katiba
2026-09-28 17:06:31
10
Manyama001 :
Sasa Makamu umejua kucheza na akili zetu na tunacheza mdundo mmoja safi sana, apo vijan kam ssi ambao hatun ajira basiiih naanz kuona mwanga, kumbe uliletwa kwa makusud ya Mungu , mmi nimlinz wako wa kwanz mtu asikuguse kabis
2026-09-29 01:14:47
9
josephmassawe342 :
ivi mm najiuliza kwan magu hakumuona huyu👆
2026-09-29 03:13:58
2
""The Matthew Jr"" :
Vijana elfu 10 kati ya vijana wa ngapi 😳😳,tupeni bima ya afya kwa wote jamani ili wananchi tuwe na uhakika wa matibabuu haya mengine yawe ziada tu 🙌
2026-09-28 17:20:22
8
Neema za Mungu :
MLINZI WAKE MBONA MZEE
2026-09-30 13:07:37
0
Seif Mohammed :
rais wang huyu mwaka wa mbele
2026-09-28 16:54:03
20
Matukuta J Matukuta :
SAMIA KAONA MBALI MNO! kwahili hakiyake openi!
2026-09-28 19:10:22
0
user818263508440 :
Huyu ndio makamu wa RAISI💯
2026-09-28 23:56:12
6
sulekh🔥 :
huyu jamaa anakitu tumuombee Kwa mungu azidi kututetea Vijana pamoja na watu wote Kwa ujumla amini.
2026-09-28 17:40:27
15
David Timotheo :
uzalendo naubunifu ndio utakap tufikisha mbali
sio alili yadarasani nakukubali mkuu
2026-09-28 20:43:44
2
kibhabha22 :
kwa maneno hamjambo
2026-09-28 19:23:35
1
Saidi Abdulbari :
me naomba msimuangushe mkuu km kasema kweli basi mh mkumbo, naibu waziri w fedha na wengine wote pambaneni na inawezekan
2026-09-28 17:20:04
9
kemal :
Hii ndio raha ya kua na serekal ya vijana alieitengeneza Dr Samia Suluhu Hassan 💯
2026-09-28 22:05:56
5
Elikana isack :
ase mungu mkubwa Hawa ndo viongoz asa ndo faida ya kutumiah viongoz vjan
2026-09-28 19:44:27
4
makido12 :
huyu tumepata kiongozi mungu tulindie huyo aje atuokoe nalivyo naumli mdogo 🤝🤝🤝
2026-09-28 19:32:42
4
Nabii Alimas :
Hotuba Bora zaidi ya makamu wa rais
2026-09-28 17:58:51
3
giddion omera :
huyu Jamaa kdg namuelewa
2026-09-28 17:38:39
4
JBGT Thobias :
nakubalii sanaà kwa mbaaliiiiiii kdg naona unakuja mkuu
2026-09-28 17:14:59
4
Johanes Joseph :
tunahitaji katiba mpya aya yote yawe sawa ni katiba mpya maana mawazo yako ni sawa lkn bila katba haya ni hewa
2026-09-29 04:15:52
1
Shija kwango :
huyu jamaa angeongezewa Engineer Hersi Said aaaaaaa tungpepea kimaendeleo miaka ya mbele
2026-09-29 06:28:55
2
Swemto Boy :
jamaa alikuwa wap huyh
2026-09-28 17:40:20
1
To see more videos from user @uhuruonline, please go to the Tikwm
homepage.