@jambotv_: VIDEO: Mabasi yanayobeba abiria katika Stendi ya Nanenane jijini Dodoma kuelekea mikoa mbalimbali yamesitisha safari asubuhi ya leo, huku madereva wakidai kuwa watarejea kutoa huduma baada ya madai yao kufanyiwa kazi. Wakizungumza jijini Dodoma, baadhi ya madereva hao wamesema mgomo huo umetokana na malalamiko mbalimbali, ikiwemo kukamatwa kwa magari yao kwa madai ya kukiuka sheria za barabarani, kufungiwa leseni zao kwa kile wanachodai kufanyika kinyume cha utaratibu, pamoja na madai kwamba baadhi ya askari wa usalama barabarani wamekuwa wakiweka mawakala katika shughuli za usafirishaji. Aidha, baadhi ya abiria wamelalamikia hatua hiyo na kuiomba Serikali kuingilia kati ili kutatua mgogoro huo, wakidai kuwa mgomo huo umewasababishia usumbufu na kuvuruga mipango yao ya safari. Hata hivyo, hadi sasa, Jambo TV inaendelea kuzitafuta mamlaka husika kwa ajili ya kupata ufafanuzi kuhusu madai hayo pamoja na kauli ya Serikali juu ya mgomo huo.

Jambo TV
Jambo TV
Open In TikTok:
Region: TZ
Tuesday 29 September 2026 06:44:00 GMT
131569
8871
275
210

Music

Download

Comments

malkia049
Vee🦋⚘🦋 :
Ngoja hii nauli nikale tu kitimoto nisha pata sababu😂😂
2026-09-29 08:20:05
39
calkid_
Calkid :
binafsi nishakasilika mimi sitaki kuongea tena😂😂😂
2026-09-29 07:23:00
105
allenraymond03
allenraymond400 :
daaaa nimemtumia demu nauli sijui itakuwaje
2026-09-29 07:34:00
73
jamal.saidi522
Jamal Saidi :
Safi sana madereva wenzangu
2026-09-29 07:41:49
40
dar_es_salaam_arusha
Mr.J.🎯DSM kkoo free_delivery :
MTANIKUMBUKA 😭😭
2026-09-29 08:56:17
21
jayden45.2
malongo jr :
ep 1 sizon 2
2026-09-29 09:57:38
0
godwnpallangyo
Godwini Pallangyo :
Jamani malori tukowap mbona hatusemi jambo
2026-09-29 07:30:32
17
zubedayo0
yuda z maganga :
majeshi yoote nimali ya CCM
2026-09-29 07:21:23
18
aquariusman84
Emma. wimbi :
fateni Sheria za usalama barabarani [Tears of joy][Tears of joy][Tears of joy][Tears of joy]
2026-09-29 07:48:32
8
dastanraymondmbwa
Dogo tz0 :
waondoe point
2026-09-29 08:22:16
0
nyarasya
[email protected] :
mtu unacheti alafu wanataka ukasome tena tabu juu ya tabu
2026-09-29 07:48:22
14
bakaridbg
Brown Mgongoa :
Bongo lala
2026-09-29 08:11:16
0
user19700914676093
Yohnchey :
My Country
2026-09-29 08:06:11
0
rosenyondo611
rosenyondo611 :
mpk dar wagone kila badi liludi sehemu yk yanakopakia
2026-09-29 07:41:41
5
bwestlabba0
B West Labba :
sasa tufanyeje maana ata nyinyi madereva wengine kweli hamuendeshi kwa usalama, kwani ajali za kijinga mnazofanya hamuoni jamani ebu dereva aongee hili pia tumepoteza ndugu zetu apo dodoma juzi juzi tu apa kwa uzembe wa dereva wa isamilo mbona hamsemi?
2026-09-29 08:49:08
1
maksensia.alex
Maksensia Alex :
kaka nimekuona
2026-09-29 09:44:14
1
mbazi66
Mbazi Mkiramweni :
sio mabasi yamegoma ni madereva wamegoma 😅😅
2026-09-29 07:26:06
6
deogratiusyudatad
deorgatius :
tz Kuna wahuni tu hakuna serikali banaaww
2026-09-29 09:43:28
1
enockezekiel977
The blues 💙 :
Serikali waonezi, wao mbona ugali wao hauguswi??!!
2026-09-29 07:58:23
5
johnson_tz
Arajick tz :
nita panda ndege nyie gomeni hadi mwezi ujao maana serikali imeshakuwa haina shida na wananchi wake
2026-09-29 07:22:14
5
boniphacejames
Boniphace James :
mgomo uendelee maana masharti Kwa dereva ni mengi kuliko mshahara anaopata dereva
2026-09-29 09:22:10
1
merry.cut0
Princess 👸 :
Na ndege pia ziwe na mgomo
2026-09-29 08:46:36
1
user23109734271678
Robby dhe don :
Nataka kufaam kwan nyie madereva Amuna mwana shelia wa kuwa saidia!?? au bass nipen kazi
2026-09-29 08:24:34
1
wizzykha5
Wizzy Kha :
WATUACHE JAMANI 😳
2026-09-29 08:26:28
2
user1886680457987
abbas juma :
dar zamu yetu lini jamani
2026-09-29 08:17:38
0
To see more videos from user @jambotv_, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About