@lumumbahospitalzanzibar: Kila mapigo ya moyo ni maisha. Tutunze mioyo yetu kwa mazoezi!" Ujumbe kutoka kwa Daktari Bingwa wa Moyo, Dkt. Khuzeima Khanbhai, Hospitali ya Mkoa ya Lumumba, Zanzibar katika Siku ya Moyo Duniani: Tenga muda wa mazoezi: Licha ya shughuli nyingi za kazi daktari anashauri kutenga dakika 45 kwa ajili ya mazoezi ili kulinda afya ya mwili na moyo wako. Fanya mazoezi na familia: Unaweza kutumia nafasi hii kufanya mazoezi na familia yako ili kuimarisha afya, kuepuka magonjwa kama shinikizo la damu na kisukari, na kupunguza msongo wa mawazo. 📍 Hospitali ya Mkoa ya Lumumba, Zanzibar 📞 0773 034 442 #WorldHeartDay #SikuYaMoyoDuniani #LumumbaHospital #AfyaYaMoyo #Zanzibar