@jasusimsanuaji: 👉WAKILI WA SERIKALI NASSARO KATUGA ANAFANYA MAJUMUISHO YA MWISHO MAHAKAMANI DW4 anasema yeye alikuwepo tarehe 23 Aprili 2025 na alimsikia mshtakiwa akisema, “Kwani tukikinukisha watatuua? Kwani si watanikamata na kunifungulia kesi ya uhaini?” This is purely treasonous intention. Inaonyesha wazi kwamba mshtakiwa alitamka au alifanya vitendo vile vya maneno akiamini kwamba anachokifanya ni uhaini. Chini ya kiapo, mshtakiwa alisema ni kweli kwamba alitamka maneno hayo kwamba, “Sanasana watatukamata na kutufunga.” Waheshimiwa Majaji, kwenye hiyo hiyo kesi ambayo nimeirejea kuhusiana na ushahidi wa mshtakiwa, ninamalizia kwa kusema ushahidi wa mshtakiwa ni “the best evidence against him.” Waheshimiwa Majaji, labda Mahakama hii Tukufu itajiuliza, kweli zile kauli zilichochea umma? Waheshimiwa Majaji, Mahakama yenu Tukufu haitapata tabu kupata jibu la kama hizi kauli ni za kichochezi au zilichochea. Waheshimiwa Majaji, upande wa Jamhuri tumeleta ushahidi wa mashahidi waliosema waliathiriwa na yale maneno. Waheshimiwa, mashahidi hao ni P6 kama PW5, P4 kama PW10, P2 kama PW7, P8 kama PW8, P3 kama PW13 na P9 kama PW14. Waheshimiwa Majaji, mashahidi hawa wote, kwa nyakati tofauti, waliiambia Mahakama hii kwamba walichocheka na maneno ya Mwenyekiti wao. Wengine ni wafuasi na wengine ni wapenzi, yaani watu wanaompenda Mwenyekiti ambaye hapa ni mshtakiwa. Waheshimiwa Majaji, katika ukurasa wa 397, shahidi ameiambia Mahakama kwamba amepanga kumsupport Mwenyekiti kwa kuungana, kupiga na kufanya vurugu kwa kuwarushia mawe. Waheshimiwa Majaji, ushahidi wa mashahidi hao wenyewe unaungwa mkono na mashahidi wa upande wa utetezi kuanzia DW1 hadi DW4. Ukimtoa DW5, ambaye alikuwa anasema, “sijui, sijui, sijui.” Wengine wote wanasema Mwenyekiti hakufafanua aliposema, “tutahamasisha uasi kuvuruga uchaguzi”; hakufafanua aliposema, “tutazuia uchaguzi.” Waheshimiwa Majaji, tunasema hawa watu walikuwa na haki ya kuchocheka, tukikopa maneno ya mshtakiwa kwamba yeye ni mtu anayeaminika. Walikuwa na haki ya kuamini na kufanyia kazi maneno ya mshtakiwa kwa kuwa anaaminiwa na kuaminika. Na ushahidi wa kwamba yeye ni mtu wa kuaminika tunaupata katika ukurasa wa 562 wa rekodi za Mahakama. 👉LIKE KAMA UMESOMA NA 👉 Follow JASUSI MSANUAJI
JASUSI MSANUAJI
Region: TZ
Tuesday 29 September 2026 16:37:44 GMT
Music
Download
Comments
Tungaraza :
Alishindwa hata kuitetea hoja uhaini. Kaishia kusema tu mshitakiwa alikuwa na nia ya kuitisha serikali.
2026-09-30 07:19:07
3
MICHAEL SALOON KAHAMA :
Tanzania yetu n nchi yenye aman tuamin kwamba Hamna historia nyingine mbaya itaenda kutokea tarehe 9 October
2026-09-29 22:38:30
0
Inta Take Aways :
Lisu alifanya utani sana alifikili Kesi i utani
2026-09-30 12:51:06
2
Osman Bey :
3-0 😁
2026-09-30 20:04:12
0
vicent victor :
redio zao za Wakina nani?sjaewa
2026-10-04 04:59:35
0
kabosho :
kwisha habari yake
2026-10-03 07:53:34
0
Hk 6% :
lisu mitano tena
2026-09-30 16:22:21
0
life bike :
2026-09-29 18:11:19
0
user maulid nchiman :
katuga mwamba
2026-09-30 14:15:33
2
Angelo :
Lissu ni sauti ya mamlaka na Ni sauti ya Umma hakika mawe yataongea
2026-09-30 16:27:35
0
To see more videos from user @jasusimsanuaji, please go to the Tikwm
homepage.