@jambotv_: VIDEO: Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, ametoa wito kwa Watanzania na makundi mbalimbali ya kijamii kuondoa chuki, visasi na kujenga utamaduni wa kuvumiliana na kusikilizana ili kulinda amani na ustawi wa taifa. Katambi ameyasema hayo leo jioni ya tarehe 29 Septemba 2026 wakati akizungumza na madereva na abiria wa mabasi ya masafa marefu katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli jijini Dar es Salaam, kufuatia vuguvugu la mgomo wa madereva wa kupinga mfumo wa kukatwa pointi za leseni. Akiwasilisha ujumbe huo mbele ya madereva na abiria waliokusanyika kituoni hapo, Katambi ameeleza masikitiko yake kuhusu kuongezeka kwa chuki zisizo na sababu kwenye jamii na kusisitiza kuwa nchi haiwezi kujengwa kwa misingi ya kutokusikilizana. Katika kuonesha jinsi makundi yote katika jamii yanavyotegemeana, Katambi ametoa mfano wa umuhimu wa ushirikiano kati ya madereva, abiria na Jeshi la Polisi. Ameeleza kuwa iwapo kundi moja litakosekana au kuacha kuwajibika, mnyororo wa uchumi na maisha ya kila siku yatasimama, kwani biashara na huduma mbalimbali zinategemea usafirishaji wa madereva. Waziri Katambi ametoa ahadi kwamba atakuwa balozi wa madereva katika kufikisha na kushughulikia kero zao zilizofungamanishwa na sheria kwenye mamlaka husika, akisisitiza kuwa Serikali inatambua mchango mkubwa wa madereva katika ujenzi wa uchumi wa taifa.
Jambo TV
Region: TZ
Tuesday 29 September 2026 19:32:04 GMT
Music
Download
Comments
Costantine Mushi :
wakae bench na pia mishaara ipande na posho
2026-09-29 23:06:51
7
DELEVA MPOLE 91 :
police ni waonevu sana
2026-09-29 19:41:14
5
katwe :
polisi watende haki sio kila kosa ni adhabu wawe wanaanza na kutoa elimu kwa wakosaji
2026-09-29 20:19:46
3
Moses White1 :
sema mama samia oyee uone
2026-09-30 04:34:32
3
Mr Reddingtone :
kwani chanzo Cha chuki na hivyo visasi mnajifanya hamvijui
2026-09-29 19:38:53
4
Monty_7 :
duuh Hadi waziri kacheka🤣🤣🤣kaona kweli watu wamechoka na police
2026-09-29 22:41:38
1
Mbilinyi :
Nchi hi nitajiri sana sio wakati dereva ksimamishwa na polisi funga camera punguza polisi barabarani jifunze Rwanda uganda wanatuzidi nn
2026-09-30 03:38:35
2
ellyssilwamba :
hapa kuna shida madeleva wanalalamikia maasikari wa barabarani alafu unaenda waziri wa mambo ya ndani ambae ndiye mwenye watu hao serikali tuwe siliasi kidogo kwahapa mnatuferisha
2026-09-30 03:10:56
0
user9835816205682 :
c c m nchi inatutoka hii
2026-09-29 21:06:17
2
karzai :
police Tanzania wanakandamiza dereva
2026-09-30 03:18:20
1
harold :
kumbe kuna haki ya kusilizwa abiria
2026-09-30 02:10:00
1
msenda plumbing services :
musitufanye sisi wajinga aya bhana sorry wakuu
2026-09-29 22:34:38
1
Agatha Kyara :
Itakuwa nzuri
2026-09-30 05:51:14
0
ROBERTH MUSHI :
hapa saa ngap vile
2026-09-29 23:34:02
1
Aman Daniel :
ukionA hivo ujue kuna chanzo
2026-09-29 19:49:01
1
lucasmwaveyah :
Kama ni hiyo ni kwa nini hamtaki kuwasikiliza wapinzani.
Ni lini ninyi kama serikali mnawapa wananchi kusikilizwa.
2026-09-30 05:49:44
0
bahd_spenco_45 :
Police watoke tuu hali ni shwariiii
2026-09-30 00:10:07
0
lyandala noah :
mbona Zambia ishakua hivyo mkuu wala hakuna shida bwana kiongozi
2026-09-29 19:55:16
0
TATA BM🦅🇹🇿(Newman) :
ILA VIONGOZI WA TANZANIA KWA SASA IPO KIMASLAHI ,OYA MAGUFURI TUTAKUKUMBUKA
2026-09-29 20:54:56
4
Maumau march Mwana wa adamu :
police watolewa wote hakuna kitakacho fanyika dereva ni mhimili mkubwa sn
2026-09-30 05:01:53
0
tinkerman :
huyu nani
2026-09-30 06:47:52
0
vumilia said :
polis hawapo fea
2026-09-30 06:12:49
0
jonte :
mutuache bwana
2026-09-30 05:04:08
0
Hunter Emmanuel🇹🇿🎯 :
Kwani polisi ndio wanaendesha magari yetu!!!?
2026-09-30 06:45:14
0
mr_emoney_tz 💲 :
chanzo cha chuki ni wao police
2026-09-29 20:01:59
0
To see more videos from user @jambotv_, please go to the Tikwm
homepage.