@jambotv_: VIDEO: Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, ameingilia kati mgomo wa madereva na abiria wa mabasi ya masafa marefu katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli jijini Dar es Salaam, huku akiagiza kupatiwa orodha kamili ya leseni zote zilizofungiwa pamoja na sababu zake. Akizungumza na madereva na abiria hao jioni ya leo Septemba 29, 2026, kufuatia mgomo wa kupinga mfumo wa kukatwa pointi za leseni na ufungaji wa leseni zao, Katambi ametoa wito wa kuwepo kwa utulivu na usikilizano ili kufikia suluhu ya pamoja. "Hakuna jamii ambayo inaweza ikafanikiwa jambo kama hamsikilizani... Kwenye zile leseni zilizofungiwa kuna wengine wamefungiwa leseni lakini kuna wengine ambao wanazungumzia swala la ufungaji leseni wasifunge polisi ziwe na utaratibu mwingine," amesema Katambi. Akiweka wazi kuhusu takwa la madereva la kutaka mfumo wa ufungaji leseni ufutwe mara moja, Katambi ameeleza ukweli kuwa maamuzi ya mfumo huo yalipitishwa na Bunge na vikao halali vya kiserikali, hivyo hayawezi kufutwa tu kwa tamko la kiongozi aliyesimama jukwaani. Katambi amewahakikishia madereva na abiria hao kuwa serikali imechukua kero na maoni yao kwa uzito na kwamba suala hilo linakwenda kufanyiwa kazi kwa pamoja na wizara zote husika chini ya uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu.

Jambo TV
Jambo TV
Open In TikTok:
Region: TZ
Tuesday 29 September 2026 20:28:54 GMT
58820
1635
69
46

Music

Download

Comments

mo__sparta
mo__sparta :
sisi madereva wa school Bus tunaomba wazazi mpunguze maji kwenye Juice za watoto
2026-09-29 23:55:56
19
joelumambo
Jo :
Kuchokonoa mambo nijadi yetu we never live peaceful.
2026-09-30 04:53:06
0
amosika6545
AMOS✅️✅️⭐️⭐️ :
jamana msikilize kwanza sio kupiga kelele
2026-09-30 10:23:42
1
mobabe2
momobabe😍😘 :
Uyu ni nan
2026-09-30 03:56:01
4
nascoba5
nascoba :
watanzania wa sasa sio wale wa enzi za ujima
2026-09-30 04:41:34
7
abduliddy6007
a"b"d"u"l .. :
serikali inatakiwa kuwa na busara sana watu wamebadilika sasa hivi
2026-09-30 04:03:37
3
aloycetemu999
Aloyce Temu :
atukutaki wwe raisi ndotunamtaka
2026-09-30 07:41:38
0
mjamaic
MJ4️⃣5️⃣ :
bongo mungu atusaidie watu wamekuwa sio waoga kabisa 🙏🙏
2026-09-29 23:42:51
5
olesomi
Ole Somi :
Uzuri wenu CCM Mmoja akinya mwingine anakuja kutawaza
2026-09-30 04:57:38
4
kingkidude
kidude :
napenda tunavyoendelea kua naujasili wakuwaambia ukweli viongozi
2026-09-29 23:42:39
4
tonny_the_guide
Tonny Tanzania :
dahhhh swala dogo tu muitane dodoma kula hela zetu 😂😂😂 dahhh kikao kimoja laki nane lesen elfu sabini 😁😁 wabunge mkoo sijui miangapi mungu tutetee
2026-09-30 05:22:59
3
sugarbates2
sugar bates :
2026-09-30 05:25:56
1
subwoofer_87
subwoofer_87 :
mnaenda kulifanyia kazi wapi? wakati mgomo ulitangazwa kabla,ina maana hamkuona athari hii?..
2026-09-30 04:30:07
2
allanmongii
Mr. Kilimo :
Na mgomo wetu umepitishwa na vikao kuufuta hapa jukwaani ni uongo!! tunachukua mapendekezo yenu tuyafijishe kwenye vikao vya uongozi wa madereva yakafanyiwe kazi
2026-09-30 06:33:53
1
editha.kokuberwa
Editha Kokuberwa :
Kwani nini maana ya maamuzi ya dharura.
2026-09-30 06:31:03
1
eliahmsemwa413
eliahmsemwa413 :
Msukuma anaakili sana yule mtu alishapinga sanaa bungen suala la madereva kukatwa point na kulipa gharama tena kwenda kusoma ila wapewe semina ambazo ztakua ni bure
2026-09-30 04:51:23
1
dikakimishamsumbwatz
Dika kimisha +225786273990 :
keshashindwa nchi hii kwani inaongozwa na nani nyuma ya pazia Kuna nani
2026-09-29 22:38:47
1
gentleamo01
gentleamo01 :
Wanatuchukulia poa
2026-09-29 20:43:30
1
ali.mvungi
ali mvungi :
ila Tz kwaiyo wabunge ndio walimaliza kufkiria nakutunga mambo kama hayo
2026-09-30 08:24:43
1
kasongohmatipan17
kasongo multdesign_furniture :
siasa mpaka kwenye chakula cha watu
2026-09-30 07:32:28
0
honestsebastian0
Honest Sebastian :
MNAANZISHA MATATIZO ILI MUYATATUE😂
2026-09-30 11:41:21
0
kelvinkeen4
Keen :
ongea chap
2026-09-30 12:39:49
0
benbariki
Tit4Tat :
Mi kwa mtazamo wangu, na maoni yangu, nadhani inabidi niweke sawa kwamba kwa maneno machache sana niseme mimi kama mm naweza kuwa na mtazamo ambao Nitapenda kusema kuwa kwa maoni yangu naona ni vema kueleza kuwa inabidi sasa niweke sawa maelezo yangu kuwa hili suala ni ambalo kwa maoni yangu naona kuwa maneno ambayo naweza kueleza kwa ufundi sana na kutokana na mawazo yangu. Sasa nimalizie kwa kusema kuwa naona mawazo yangu ambayo yanaeleza kuwa mtazamo ambao mimi binafsi ningetamani kusema kuwa inabidi maelezo haya ambayo nayatoa ni kwamba, kwa maneno machache nieleze kuwa naweka wazi ya kwamba maoni yangu na mawazo yangu naeleza kuwa mtazamo huu ni kueleza kuwa sina la maana ndugu zangu.😁
2026-09-30 12:38:13
0
raajyr
Mr. Ramsey :
wananchi hawataki maneno ya kisiasa nyoosha maelezo gusa mambo wanayotaka kwa sasa then tafuteni suluhu yakudumu
2026-09-30 07:41:36
0
uncle.kp4
UNCLE KP :
sasa huyuuuuuu
2026-09-29 22:04:39
0
To see more videos from user @jambotv_, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About