@jambotv_: VIDEO: Asubuhi ya leo tarehe 30 Septemba 2026, simanzi imetawala katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli jijini Dar es Salaam baada ya Bwana Harusi aliyekuwa akisafiri kuelekea wilayani Kahama mkoani Shinyanga kwa ajili ya sherehe ya Send-off iliyopangwa kufanyika kesho, kukwama na kumwaga machozi kufuatia mgomo wa madereva wa mabasi ya masafa marefu. Bwana Harusi huyo ameeleza kuwa alikata tiketi ya Shilingi 70,000 kutoka kwa wakala wa mabasi kwa ahadi kwamba gari lingeondoka saa 12:00 asubuhi, licha ya wakala huyo kujua fika kuwepo kwa mgomo huo. Baada ya safari kukwama, msafiri huyo alimfuata wakala huyo ili arudishiwe fedha zake atafute usafiri mbadala, lakini wakala alikataa na kumtaka aende Polisi akidai kuwa hilo ni janga la kiserikali. Ameeleza kuwa ndugu na wageni kule Kahama tayari wameshajikusanya, hivyo kuchelewa kwake kunatishia kuvunja sherehe hiyo na kusababisha hasara kubwa. Jambo TV ilipopiga simu kwa mwakilishi wa kampuni hiyo ya basi ili kuhoji sababu za kutosafirisha abiria wala kurejesha nauli, mwakilishi huyo alidai kuwa mgomo huo ni "janga la taifa" na kwamba kampuni pia imepata hasara kwani magari yapo tayari lakini madereva ndio waliogoma kuendesha. Kukwama huko kwa abiria kunatokea ikiwa ni siku moja tangu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, alipofika na kuzungumza na madereva pamoja na abiria kituoni hapo jioni ya Septemba 29, 2026 kufuatia mgomo wa kupinga mfumo wa kukatwa pointi za leseni. Katika kile kinachoonekana kuwa mfupa mgumu, Waziri Mkuu wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, anatarajiwa kufika katika stendi hiyo leo kuzungumza na madereva na abiria ili kutafuta ufumbuzi wa malalamiko hayo.
Jambo TV
Region: TZ
Wednesday 30 September 2026 07:05:11 GMT
Music
Download
Comments
👑𝑸𝑼𝑬𝑬𝑵 𝑶𝑭 𝑪𝑯𝑨𝑰☕️✨. :
MBONA MELI ,BOTI NA NDEGE ZIPOO JAMANI ACHENI MADEREVAAA WAPUMZIKE [Tears of joy][Tears of joy][Tears of joy][Tears of joy]
2026-09-30 09:06:34
5
🍎𝐍𝐢𝐡𝐚𝐧🍎 :
Namuonea huruma jmn🥺🥺
2026-09-30 08:22:25
42
Mathias Home Decoration Desgn :
kwa gharama zozote siungepanda ndege asee
2026-09-30 07:58:21
27
Mr Thinker :
watu wamepata sauti ya kufanyia challenge mjin
2026-09-30 08:11:50
60
Formen Tz :
Natafuta comment ya bi harusi 😅😅
2026-09-30 08:10:15
14
Angelica🧚 :
hiyo ndoa tuiombee tu daah,bwana harusi ndio huyo
2026-09-30 08:41:22
7
KWITHIRA PLUS :
wana challenge voice mko wap mbn mwaniangusha
2026-09-30 09:09:06
0
Aden Vales 🌊 :
Duuuh kama haiko kwako unaweza kudhani anafurahisha lakin kiukweli hili jambo linauma sana😰😰😥😥🙌🙌🙌
2026-09-30 08:05:00
32
Halliem🍒🩵 :
challenge hyooooo 😂😂😂😂😂
2026-09-30 09:10:33
0
Miss G❤️ :
New Challenge in town😂😂
2026-09-30 09:00:23
0
chusse78boy :
unajua nacheka kwann
2026-09-30 07:23:03
16
Gdence Auto Spare Parts :
Last born bwana
2026-09-30 07:42:52
5
Razack R Kasimu :
Hii watapita nayo kwenye sound
2026-09-30 08:00:55
32
Pretty T❤️ :
Mm ndo bib harus
2026-09-30 08:38:07
7
black horse :
😁 eeh basi tena siendi tena kahama kma sauti ndiyo hizo
2026-09-30 07:41:49
6
flowergirl :
keshatapeliwa😳
2026-09-30 08:22:59
6
Abooy :
hi hali hua inaumiza sana majeti wanautepel mwengi sana wa maneno
2026-09-30 08:14:17
5
🦋 Unworthy 🐞🦋 :
sawaaa 😅😅
2026-09-30 09:05:56
0
Phina Ndagula :
Kama kuna mgomo na wanajua kwa nini wachukue hela za watu serikali ilione hilo haijakaa sawa
2026-09-30 09:24:32
0
Salma Leon :
na ss wa sup😂
2026-09-30 08:15:22
0
Jackson J. Marko :
Mliwakatia ticket za nn wakati mnajua kuna issue ya kitaifa??
2026-09-30 07:50:08
3
bosslady :
wahiii kakaaa harusi bdo tunayoo bwana harusii usjal🤣🤣
2026-09-30 09:08:26
1
sulu1103 :
shemeji usilie dada yupo ana kusubili
2026-09-30 08:57:08
1
Hashimmoh’d :
Misifanye challenged please 😁
2026-09-30 08:12:25
4
Dourdour 🦋🫶🏻. :
Watu wa challenge😂🤌
2026-09-30 08:47:43
3
To see more videos from user @jambotv_, please go to the Tikwm
homepage.