@jamiivoice_: HABARI: Hali ya sintofahamu imejitokeza leo jijini Arusha baada ya wafanyakazi wapatao 70 wanaokusanya mapato ya maegesho ya magari kugoma, wakidai kutolipwa mishahara kwa muda wa miezi miwili pamoja na kutokuwa na mikataba rasmi ya ajira. Wafanyakazi hao, wanaodai kufanya kazi chini ya moja ya kampuni zinazohusika na ukusanyaji wa mapato ya maegesho, wamesema wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali za kikazi, ikiwemo madai ya kutowasilishwa kwa michango yao ya NSSF kwa takribani miaka miwili. Wamesema katika kazi zao hulazimika kuhudumia zaidi ya magari 300 kwa siku, huku wakifanya kazi katika mazingira ya jua na mvua. Pia wamedai kupewa malengo ya ukusanyaji wa mapato, na kwamba mfanyakazi anayeshindwa kufikia lengo hilo hudaiwa kunyang’anywa mashine ya kukusanyia mapato. Kwa mujibu wa wafanyakazi hao, kutolipwa mishahara kwa wakati kumeathiri maisha yao na familia zao, hususan katika mahitaji ya chakula, malazi, ada za watoto na mahitaji mengine muhimu. Wameiomba Serikali, hususan Wizara yenye dhamana ya Kazi na Ajira pamoja na mamlaka nyingine zinazohusika, kuingilia kati na kushughulikia madai yao kuhusu malipo ya mishahara, mikataba ya ajira na michango ya NSSF. Aidha, wameitaka mamlaka husika kuchunguza uwezo na utendaji wa kampuni inayodaiwa kuwahudumia pamoja na utekelezaji wa tenda ya ukusanyaji wa mapato ya maegesho katika Jiji la Arusha. Juhudi za Jamii Voice kupata majibu kutoka kwa kampuni hiyo na mamlaka husika zinaendelea.
Jamii Voice
Region: TZ
Wednesday 30 September 2026 10:38:51 GMT
Music
Download
Comments
Joel :
pole ma mparee
2026-09-30 13:38:27
4
𝔸𝕘𝕒𝕥𝕙𝕒 𝕃𝕚𝕠𝕟𝕖𝕤𝕤 🦁 :
Hiyo laki Naombeni nimlipe huyo mama aje ofisini kwangu akae🤎 asizunguke
2026-09-30 16:51:54
8
Wagon :
magari 350 maninaa hii ndio tanzania
2026-09-30 16:09:10
7
Daniel Frank :
CCM OYEEEEEEEEEEEEEEEEEE
2026-09-30 15:14:59
1
juma issa :
yaan unadai kisha unapeleka hela si uchukue hela uliokusanya
2026-09-30 15:34:09
4
rayshkeykeyraa :
kila mtu atagom kwa wakat wake
2026-09-30 12:26:07
11
mosses🐾🚛 :
nasemaje? nasemaje? wote tutaongea lugha moja
2026-09-30 13:36:29
5
𝕃𝕒𝕦𝕣𝕖𝕟𝕥 𝕤𝕒𝕞𝕚𝕝𝕒 :
hizo machine zinafaa kufanya uwakala wa bank?
2026-09-30 19:14:52
0
Bai :
Hiyo ndio ccm mlio hitaka.
2026-09-30 14:40:32
2
Baraka :
Kampuni za Kitapeli hizo wanapewa Tender na hawawezi lipa watu
2026-09-30 17:01:43
1
big boy :
hiyo ndio kuisoma namba
2026-09-30 14:33:49
1
Josse nderingo :
ndio maana gari zingine wanafosi wanatumulika tukiwa fole🥹 gari yangu Kila mahali makutaga inadaiwa wakati uko cjapak
2026-10-01 09:23:15
1
Godedivine empire :
nimemuona Mama g
2026-09-30 17:36:13
1
Ethan Maro :
yaani wenye magari Arusha tunateseka sana,ukitembea tu unaandikiwa
2026-09-30 15:52:51
1
peter kandidi :
poleni msilipwe kabisaa
2026-10-01 08:00:36
0
aronmtui709 :
Serikali angalieni huu ni zaidi ya unyanganyi
2026-10-01 11:03:59
0
marikigft😀🥰 :
yona atashuka
2026-09-30 11:18:29
0
Mopao :
Mama pole sana
2026-10-01 21:51:45
0
RICHS👨🔧💫 :
Kwana scaner yenyewe inasemaje??
2026-10-01 05:38:05
0
Mrs frank :
nimeona gar yetu ya nyumbn kiaz kitamu jmn
2026-10-01 09:15:31
0
AveMaria :
wanatubambikizia makosa sana. jaman mimi nimekuta nadaiwa zaidi ya laki na nusu
2026-10-01 08:29:21
0
D A B Z I E 🇿🇲🇹🇿 :
ndomana mnatoza ushuru hadi magari ya watu kwenye nyumba zao ,huu ni wizi kama wizi mwingne tu
2026-10-01 06:25:40
0
RICHS👨🔧💫 :
na kama ni lazaima yascaniwe magari mia mbili kwa siku wanauhakika hayo wa hayo magari yanapark yote??
2026-10-01 05:40:57
0
Baharia Mkombozi :
😁nchi ngumu hii
2026-09-30 11:32:38
0
To see more videos from user @jamiivoice_, please go to the Tikwm
homepage.