@drtediwellness: Mwanzoni ilikuwa kawaida tu. Nilianza kupata maumivu chini ya tumbo, kuchomachoma wakati wa kukojoa na kwenda chooni mara kwa mara. Nikawa natumia dawa, dalili zinapungua kwa muda… halafu zinarudi tena. Nikajikuta naishi hivyo karibu kila siku. Kadri muda ulivyokuwa unaenda, hali ilizidi kuwa mbaya. Maumivu yakaanza kuwa makali zaidi, nikapata miwasho na uchafu usio wa kawaida. Wakati mwingine hata tendo la ndoa lilikuwa linakuwa na maumivu. Nilizunguka hospitali nyingi sana. Vipimo, dawa tofauti tofauti… Kila mtu alikuwa na ushauri wake, lakini mimi ndiye nilikuwa nabeba ule uchungu kila siku. Kibaya zaidi, watu wengine walikuwa wakisema: "Ni U.T.I tu, si kitu kikubwa." Lakini hawakujua nilivyokuwa nateseka. Kuna kipindi nilikuwa naogopa hata kutoka mbali kwa sababu nilihisi nitahitaji kukojoa kila muda. Maumivu ya chini ya tumbo na hali ya kutokuwa comfortable vilinifanya nichoke sana. Nilianza kujiuliza: "Je, nitawahi kuwa kawaida tena?" 💔 Mpaka siku moja nikaamua kuacha kutuliza dalili tu na kuanza kulitafuta chanzo cha tatizo kwa umakini. Nikaelekezwa namna sahihi ya kufuatilia tatizo la U.T.I na P.I.D, vipimo vinavyofaa na hatua za kuchukua kulingana na chanzo. Siwezi kusema ilikuwa siku moja tu nikapona… Lakini taratibu nilianza kuona mabadiliko. Maumivu yakaanza kupungua. Miwasho ikapungua. Kukojoa kwa maumivu kukaanza kuisha. Nikaanza kujisikia comfortable tena. Na taratibu nikaanza kurudisha amani yangu. ❤️ Nimeandika hii story kwa sababu najua kuna mwanamke hapa anapitia hali hii kimya kimya. Usipuuze maumivu ya chini ya tumbo, uchafu usio wa kawaida, maumivu wakati wa kukojoa au maumivu wakati wa tendo. Dalili hizi zinaweza kuwa na sababu tofauti na zinahitaji tathmini sahihi. Kama umewahi kupitia hali kama hii au bado unapambana nayo… Niambie kwenye comment: U.T.I au P.I.D imewahi kukusumbua kwa kiwango gani? 💔👇 #PID #UTI #AfyaYaMwanamke #AfyaYaUzazi #WomenHealth
tedinaturalproduct075_6883106
Region: TZ
Wednesday 30 September 2026 12:15:21 GMT
Music
Download
Comments
There are no more comments for this video.
To see more videos from user @drtediwellness, please go to the Tikwm
homepage.