@veriafya: Akizungumza na Clouds Media, Dkt. Emmanuel Baida, Bingwa Bobezi wa Watoto kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili anaeleza kuwa kulia kwa mtoto mchanga ni njia yake ya kuwasiliana na mara nyingi huchangiwa na njaa, kwani watoto chini ya miezi mitatu wanahitaji kunyonya sio chini ya mara 8 kwa masaa 24 (ikiwemo usiku). Pia husababishwa na gesi tumboni inayoweza kupunguzwa kwa kumweka mtoto vizuri mtaani/kifuani na kumfanyia mazoezi mepesi au massage. Hata hivyo, anasisitiza kuwa mtoto anapolia kwa sauti kubwa mfululizo bila kutulia (hata akimnyonyesha), hiyo ni ishara hatari na inahitaji kumwona mtaalamu wa afya haraka.