@morogoroyetu: Serikali imefanya uwekezaji mkubwa wenye thamani ya Shilingi Bilioni 220 kuimarisha huduma ya majisafi katika Manispaa ya Morogoro. Naibu Waziri wa Maji Mhe. Kundo Andrea Mathew (Mb) amesema hayo Oktoba 1, 2026 katika ziara ya kikazi mkoani Morogoro akikagua uboreshaji wa bwawa la Mindu. Amesema bwawa la Mindu ni mkombozi kwa mji wa Morogoro kwa sasa licha ya kuwa na vyanzo vingine vya maji. “Nafahamu tunavyo vyanzo vingine kama mito na visima vinavyochangia ongezeko la uzalishaji wa maji lakini bado tuna upungufu wa lita milioni 39 hivyo kutokana na mkakati wa serikali katika suala la upatikanaji wa maji bado tunaendelea na utekelezaji wa miradi mingine mikubwa kupata maji ya uhakika” Mhandisi Kundo amesema. Ameongeza inawezekana kuwa na mbadala wa nishati lakini haiwezekani kuwa na mbadala katika upatikanaji wa maji hivyo wananchi wawe wazalendo katika kulinda miundombinu na vyanzo vya maji kwa wivu mkubwa kwani ni aibu kwa mkoa wa Morogoro wenye vyanzo vingi vya maji vya uhakika vinavyolisha mikoa ya Pwani na Dar es salaam kukosa huduma ya maji. Amesema kiasi cha shilingi Bilioni 9.1 kimetolewa na serikali ili kulipa fidia kwa wananchi ambao walipisha maeneo yao kwajili ya utekelezaji wa shughuli za uhifadhi wa eneo la bwawa hilo. #Morogoro #Morogoroyetu #Maji cc @moruwasa @wizarayamajitz @jumaa_aweso @eng_mwajuma.waziri9 @wamiruvu_basin

morogoroyetu
morogoroyetu
Open In TikTok:
Region: TZ
Friday 02 October 2026 05:33:08 GMT
11021
204
8
12

Music

Download

Comments

magadaughter0
♍️ 🦋 :
😂😂apo kwanza nicheke
2026-10-02 17:21:25
1
kindambjr
kindamba jr :
yupo mh Abdur Aziz Abood aka ngano kira ki2 kitakua poa babu yangu uyooo
2026-10-02 07:41:35
2
sameerparkar31
sameerparkar31 :
Maji halitaweza kutatuliwa hata tufanyeje, mji kama morogoro tukose maji kweli!!!hizo zote ni siasa tu
2026-10-02 16:03:57
1
030joshua.philipo
030Joshua Philipo :
Huyu,,mama tunae tunatamba nae,,ishu siyo rais ishu na ma-rc ila queen namkubali,,sana
2026-10-02 13:48:12
1
fuadabdallah18
fuadabdallah26 :
Bado Hali ya maji mjini ni shida
2026-10-02 09:21:02
0
tinomkenda
tinomkenda :
Mzee elezea mnatatuaje changamoto acha kuimba mapambio wakazi wa mindu hawana maji we unaleta siasa za ajabu ajabu
2026-10-02 18:44:50
1
regnetha.wagofya
Regnetha Wagofya :
Mkundi mwisho hakuna maji ya bomba
2026-10-02 19:25:02
0
hassanabdallahnyanya
Hassan Abdallah Nyanya :
hizo pesa niiteni niwaleni mchongo mkakati wa mradi chanya wa maji, kwn hizo pesa najua mtazipiga
2026-10-02 18:00:50
1
To see more videos from user @morogoroyetu, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About